Na: Moshy Kiyungi,Dar es SalaamWapenzi wa muziki wa kizazi kipya duniani hususan Afrika, kundi la P-Square limeshika nafasi ya simulizi kufuatia kazi zao kukubalika. Vijana hao wawili wa toka nchini Nigeria, Peter Okoye na Paul Okoye wanaounda kundi maarufu linalojulikana kama P-Square. Vijana hao wanaelezwa kuwa licha ya kufanya muziki, ni wafanyabiashara wakubwa wa mafuta. Historia ya mapacha Peter na Paul inaeleza kuwa walizaliwa Novemba 18, 1981 jijini Lagos, Nigeria. Walianza masomo katika shule ya sekondari ya Mtakatifu Murumba ambayo ilikuwa ni shule ndogo ya Kikatolic huko Jas, nchini Nigeria. Mapacha hao walijiunga na shule ya muziki pamoja na maigizo ambapo walikuwa wakiimba na kucheza kwa kuwaiga akina Machael Jackson, MC Hammer na Bobby Brown. Mwaka 1997 walianzisha kundi lililojulikana kwa jina la Smooth Criminal ambapo walikuwa wanacheza ‘Break dansi’. Kundi hilo lilianza kama kigenge cha mtaani kilichojulikana kwa majina ya MMMPP (M Clef a.k.a. Itemoh, Michael, Melvin, Pete... Continue reading ->
0 Comments