Habari hizo zilianza kuzagaa wakati waliposafiri kwenda Nairobi na Romy miezi michache iliyopita
Dar es Salaam. Mwanamitindo Jacquline Wolper amefungukia ukaribu wake kaka wa mwanamuziki Diamond, Romy Jons.
Wolper amesema watu wengi wanadhani natoka na Romy kwa ule ukaribu wa kufanya kazi pamoja wakati mwingine.
Amesema habari hizo zilianza kuzagaa wakati waliposafiri kwenda Nairobi na Romy miezi michache iliyopita.
“Kwanza niseme tu watu wazindoe zile fikra za mimi na Romy kuwa ni wapenzi kitu ambacho hakiwezekani na sio kwamba hafai ni haiwezekani tu.
"Nimegundua watu wanapenda kuunganisha matukio sana hii ni kutokana na safari moja ya Nairobi nilisafiri na Romy kikazi hapo naona watu ndipo walipoanza kuzusha habari zao hizi,” alisema Wolper.
0 Comments