Msanii wa vichekesho Tabu Mtingita amzungumzia madai kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Serengeti boy.
Dar es Salaam. Msanii wa vichekesho Tabu Mtingita acharuka na madai ya kuambiwa anajihusisha kimapenzi na kijana mwenye umri mdogo ajulikanaye kama Lex gitaa.
Tabu kwa sasa amekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii hasa Instagram amesema watu wanamzushia kutokana na kuonekana na mwanaume mwembamba ikiwa yeye ni mnene basi wanaanza kusema ni ‘Serengeti boy’.
Hata hivyo Tabu amesema Lex gitaa anayedaiwa ni mpenzi wake, huyo wakati mwingine huwa anamtumia katika Cameraman wa kuedit kazi zake.
Kwa upande wa Lex gitaa amesema amesikia habari za kuambiwa anatoka kimapenzi na Tabu, ila watu wajue wao ni marafiki na alitokea kukubali kazi ya Tabu na Tabu alitokea kupenda kazi ya Alex na huwa wanashirikiana katika kazi yake ya muziki.
0 Comments