Muimbaji mkongwe wa taarabu Khadija Kopa ‘Malkia wa Mipasho’ ameshangawa na tabia ya wanawake wengi kushinda mitandaoni wakiposti picha bila kujali muda wa kujifunza mambo mengine.
Khadija Kopa
Akizungumza na gazeti moja hivi karibuni ,Kopa alisema,wanawake wengi wa sasa wamehamishia maisha mitandaoni ya kijamii na kusahau familia zao jambo ambalo linaongeza mmomonyoko wa maadili kwa jamii.
“Wanawake wenzangu tunapokwenda siko kwani kutwa nzima tuko mitandaoni kushindana kupost picha, hili kwangu naliona kama tatizo kwa sababu hawapati muda wa kukaa na familia zao kujifunza mambo muhimu jambo ambalo ni hatari” alisema Kopa.
Aidha Kopa alisisitiza pamoja na mitandao kuwa sehemu moja ya kujiingizia kipato lakini ifike mahali wanawake watambue wajibu wao na kuitumia vyema mitandao hiyo hasa kuwapatia riziki na si mashindano kama ambavyo imezoeleka kwa sasa.... Continue reading ->
0 Comments