Msanii wa Muziki, Nuh Mziwanda amesema kuwa hawezi kumsaidia ChidBenzi labda msanii huyo ndio anaweza kumsaidia yeye.
Nuh Mziwanda amesema kuwa anamheshimu sana Chidi Benzi hivyo hawezi kumuongelea vibaya na akikosea msanii huyo anaweza akamchana hata nusu saa.
"Chiddi Benzi mi siwezi kusema eti aje studio mimi nimsaidie yule ni brother alikuwa noma Ilala kwahiyo yeye akija studio kwangu mimi anakuja kunisaidia kuweza kupata truck na yeye itakuja tu itafanyika si unajua kila kitu ni mipango na inatokeaga tu automatically mizuka haijatokea ikitokea mizuka free kwasababu ile ni studio yake," Nuh ameiambia Wasafi Tv.
0 Comments