Ndoa ni maisha ya amani na upendo ingawa kuna baadhi ya wengine imekuwa ni tofauti
Wapo ambao tangu wameingia katika ndoa hawafurahii ndoa zao na kujikuta kila iitwayo leo ni kilio hawajawahi kuwa na furaha.
Unapaswa kujua wewe hukuolewa kuwa mtumwa wa ndoa yako usikubali kuwa ni mwenye huzuni kila siku.
Mwanaume mwenye mapenzi na wewe hawezi kusababisha kila siku uwe wa kukosa amani.
Kuna wengine wamegeuzwa ni sehemu ya kupigwa kila kukicha ama kufanyiwa unyanyasaji.
Wengine hukimbizwa hata kwa kisu na kutamkiwa maneno mazito lakini wamo ndani ya ndoa.
Unajua hata mume kurudi asubuhi ni maumivu makala ambayo mwanamke anayapata hasa kwa yule anayekupenda.
Ndoa yako ikifikia kwenye hatua mumeo anakuambia atakuchinja ama kukuua usichukulie ni maneno ya mazoe chukua hatua.
Napatwa ugumu kidogo kujua ni kipi ambacho kinakufanya kung’ang’ania sehemu ambayo hauishi kwa amani kila kukicha unakimbizwa na panga lakini bado unaendelea kusema una ndoa.
Nataka kukujulisha tu ukiona mume wako anakupiga hadi anakusababishia majeraha zaidi ya mara nne na wengine hadi kulazwa ni vizuri ukachukua hatua nyingine hapo hakuna ndoa.
Ngoja nikupatia mfano kuna hawa wanandoa wamekuwa wakifukuzana wakati mwingine anamtamkia maneno magumu kuwa atamuua na mwisho wa siku waliuana.
Kuwa makini na sentensi kama hizo na kuchukua hatua ukifikia hatua hiyo mume anakuambia nitakuua bora uiache hiyo ndoa na kuondoka.
Hatua mojawapo ambayo unaweza kuichukua ni kuwajulisha viongozi wako wa dini ama wazazi wa pande mbili kile ambacho anakufanyia.
Ukiona ameonywa kwa zaidi ya mara tano na tabia zake hazitaki kubadilika jua hapo hakuna ndoa.
Baadhi ya wana ndoa hawajui haki zao na kuchukulia kuwa ndoa ni kifungo ambacho hata ukifanyiwa mateso uendelee kuvumilia.
Ndoa ni maisha ya upendo na amani na wote kufurahia na sio kumsababishia mwenzako mateso.
0 Comments