WATU 10 WAFARIKI KWA KUVUTA MOSHI WA JENERETA KWENYE SHEREHE YA HARUSI

Watu 10 wamefariki nchini Nigeria baada ya kuvuta moshi kutoka kwenye jenereta walipokuwa katika sherehe ya harusi kusini mwa nchi hiyo.

Watu wengine 30 waliokuwa kwenye harusi hiyo wamelazwa hospitalini wakiwa na shida za kupumua. Polisi wametaja tukio hilo kama lisilokuwa la kawaida na kuanza uchunguzi wa kina kuhusiana nalo.

Mkuu wa Polisi katika jimbo hilo la Imo amesema kwamba uchunguzi wa awali umebaini kuwa waathiriwa, ikiwemo wazazi wa bibi harusi, walivuta moshi kutoka kwenye jenereta walipokuwa wakilala baada ya sherehe ya harusi.


Post a Comment

0 Comments