KWANINI VITA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA HAIISHI??

Uamuzi uliotolewa na mahakama Kuu nchini Kenya dhidi ya wanaharakati wanaopinga mapenzi ya jinsia moja unaonekana kuwa ni mwanzo wa mapambano ya utetezi wa haki ya wanaojihusisha katika mahusiano hayo.

Ingawa kuna mengi ya kujivunia katika mapambano hayo ya kutafuta usawa licha ya uwepo wa changamoto za kurudishwa nyuma.Kelvin Mwachiro ameandika.

Miaka 13 iliyopita, nilikuwa sifikirii kuwa Kenya inaweza kufika hatua hii , jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja kwenda mahakamani na kupambania haki yetu. Tuna safari ndefu bado.

Kizazi hiki kinia jumuiya ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ambao ni werevu na wanajaribu kuhakikisha kuwa wakenya wanajifunza kuwapenda na kuwakubali kama walivyo.

Miaka 13 iliyopita, nilijiambia mwenyewe kuwa sitakubali kuishi katika jamii ambayo inawatenga watu wengine.

Sitaki kuigiza kuwa mtu wa aina fulani katika mahusiano au ndoa ili niwafurahishe wazazi wangu au ndugu zangu wakati si kweli.

Nilitaka kuwa na furaha mimi kama mimi kwa namna nilivyo.

Baadhi ya marafiki zangu wananisifia kwa kuwa mwerevu baada ya kujitangaza hali yangu.

Ilinichukua muda mrefu kuwaelewa ni nini walikuwa wanamaanisha kwa sababu nilikuwa mimi tu mwenyewe na sio kama nilikuwa mwerevu zaidi ya wengine.

Nina bahati kwa kuwa ninaishi mtaa ambao watu hawajali maisha ya watu wengine.

'Kushangaliwa na Minong'ono'

Nimefanya kazi katika taasisi mbalimbali ambazo wanaheshimu jinsia ya mtu.

Sijawahi kubaguliwa au kunyanyasa kwa namna yeyote.

Sijawahi kushindwa kupata nyumba, ajira au kukosa huduma yeyote kwa sababu mimi ninapenda mapenzi ya jinsia moja.

Nina bahati kwa kweli .

Lakini kuna watu wengi kama mimi ambao wamepitia kwenye manyanyaso na kubaguliwa kwa sababu ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Ninafahamu kuwa kuna unyanyasaji mkubwa dhidi yetu.

Hivyo vitisho vipo kwangu pia.

Lakini nikiwa kama mtu ambaye niko katika jumuiya hiyo ya mapenzi ya jinsia moja, tumejifunza kujitengenezea uhuru baina yetu ili kuwa sisi.

Tunajivunia mapenzi yetu licha ya kuwindwa. Tuko huru lakini bado tuna hofu.

Nilipokuwa kijana mdogo , ndio wakati nilipokuwa ninajificha hisia zangu za mapenzi ya jinsia moja kwa sababu nilihisi nipo peke yangu.

Hakuna mtu ambaye niliweza kumkimbilia kupata msaada akanielewa jinsi ninavyojisikia.

Nilikuwa mkiwa.

Leo, Kuna jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja nchi nzima wanaowaunga mkono , kuwahamasisha na kupendana.

Ilikuwa mwaka 2016 ambao walikuwa wanafanya kampeni ya kufungua kesi ya ubaguzi wa wapenzi wa jinsia moja.

Miaka ya nyuma, nilikuwa naona kama ninaota nilipokuwa nasikiliza hukumu ya kesi hiyo ambayp sasa inafahamika kama kanuni ya 162.

Harakati hizi zilikuwa zilikuwa zinakabiliana na sheria ambayo ilikuwepo muda mrefu uliopita.

' Mapambano ya jinsia moja'

Mappambano ya wapenzi wa jinsia moja yamekoma.

Mapema , mwezi Februari mwaka huu, hukumu hiyo ilihairishwa .

Tulihangaika kupata waandishi wa habari kupata nafasi ya kuandikwa kwa taarifa zetu za kutetea haki ili kuhamasishana.

Tumefanikiwa katika hili.

Tulikuwa tunataka hukumu.

Tulikuwa tunataka kushinda kwa nguvu zote, na tulikuwa na katiba nzuri ambayo iko upande wetu.

Ingawa tulijua kuwa tutashindwa.

Tulihudhuria mahakamani kusikiliza jinsi kesi ilivyokuwa inaendelea huku wengine wakipata taarifa kupitia vyombo vya habari.

Tunamshukuru Mungu kwa teknolojia!

Mgogoro ulianza pale kesi ilipohairishwa.

Maumivu ya kushindwa kesi.

Watu walianza kupiga kelele nje ya mahakama.

Ilikuwa ni wakati ambao tulitoneshwa majeraha yetu.

Lakini bado tuna nia ya kupambana juu ya jambo hili.

Hata kama sio leo lakini ukweli ni kwamba katika mfumo huu inabidi twende taratibu na kutoogopa kubadilika ni ushindi pia.

Miaka 13 iliyopita. Sikutarajia kuwa nitaweza kutembea katika korido za mahakama kuhamasisha utetezi wa wapenzi wa jinsia moja.

Sio wengi kati yeti ambao wameweza kufanya harakati hizi. Lakini sisi tumeweza.

Ubaguzi dhidi yetu utaendelea kwenye mitandao ya kijamii na sehemu za kuabudia, na unyanyasaji dhidi yetu bado utaendelea kuepo.

Bado unyanyasaji wa aina mbalimbali utaendelea kuepo dhidi yetu.

Lakini vilevile harakati za kupambania haki za jumuiya yetu zitaendelea nchini humu.

Ninajua kuwa tutawakilisha maumivu tuliyonayo baada ya siku chache zijazo.

Ninapata faraja nikiona wanaharakati wengine wakiinuka ili kutetea haki za watu wenye mapenzi ya jinsia moja.

Nilipokuwa na miaka 16 nilijihisi kuwa niko peke yangu mwenye hisia za namna hii lakini kumbe tuko wengi:

Ninataka kumwambia kijana wa miaka 16 sasa kuwa tuko kwenye mapambano hayohayo na kwa upendo , ingawa bado tupo nyuma.

Angalia tu ni umbali gani tumepiga kwa miaka 13.

Post a Comment

0 Comments