Na CHRIS ADUNGO
KAHABA Michele Anne Mason almaarufu ‘Kendra Lust’ amemtaka mwanasoka wa Bayern Munich, James Rodriguez, 27, kumtwaa rasmi na kumfanya wake wa halali.
Ingawa wawili hao walivishana pete za uchumba mnamo Julai mwaka jana, uhusiano wao ulikatika ghafla baada ya Rodriguez kuanza kukitalii kisima cha mwanamitindo mzawa wa Urusi, Helga Lovekaty ambaye sasa ametishia kumtema kiungo matata mzawa wa Colombia.
Hatua ya Hegla inachochewa na maamuzi ya Rodriguez kuanza kumnyemelea pia mwanamitindo mashuhuri kutoka Venezuela, Shannon de Lima.
Licha ya kufahamu kwamba Rodriguez amepata hifadhi mpya ya penzi lake katika nyoyo za Helga, 26, na Shannon, 31, Kendra ameapa kuwasha upya mwenge wa uhusiano wake na nyota huyo.
Rodriguez alianza kutoka kimapenzi na Shannon mnamo Januari 2019, miaka miwili baada ya kichuna huyo kutemana na mwanamuziki maarufu mzawa wa Amerika, Marc Anthony, 51.
Kendra ambaye ni mwanamitindo mkongwe mzawa wa Amerika, amekuwa akimsifia Rodriguez kwa weledi wake katika sanaa ya kupiga miereka ya chumbani kila anapoazimia haja ya kukitalii kisima chake.
Rodriguez alishawishika kutoka kimapenzi na Kendra, 40, baada ya kuvutiwa na ukubwa wa makalio ya hawara huyo ambaye licha ya ukongwe kumtambalia, bado anasifika sana kwa umahiri wake katika michezo ya chumbani.
Rodriguez ambaye pia amewahi kuhusiana na mwigizaji Mellisa Peregrym kimapenzi, alianza kuhusiana na Helga baada ya kutemana na Daniela Ospina aliyedumu naye katika ndoa kwa miaka sita.
Mwezi uliopita, Rodriguez alikiri kuteswa hisia na penzi la zamani la Daniela ambaye siku hizi si mwepesi tena wa kupakia mitandaoni picha alizopigwa kwa pamoja na fowadi huyo anayehemewa na Arsenal, Chelsea, Man-Utd, PSG na Napoli.
Japo Kendra amesisitiza kwamba duka lake lingali wazi kwa Rodriguez, Helga kwa sasa analitaka dume lake kukatiza kabisa mawasiliano na Kendra pamoja na vipusa wengine wanaomwania, la sivyo, naye ajiendee zake.
Licha ya kutalikiana na Daniela, Rodriguez atasalia na jukumu kubwa la kutimiza maslahi yote ya Salome, mtoto ambaye alijaliwa kumpata katika uhusiano wake wa kimapenzi na kipusa huyo mwenye umri wa miaka 27.
Kwa mujibu wa gazeti la Fox Sports, Cristiano Ronaldo ndiye kuwadi aliyemrai Helga kujipa kwa Rodriguez ambaye alitamba sana katika fainali za Kombe la Dunia za 2014 nchini Brazil.
Kubwa zaidi ambalo limewaduwaza mashabiki wa Rodriguez ni jinsi alivyomudu kumridhisha Kendra, kahaba ambaye anajivunia kufyatua filamu za ngono kama vile F*** Me Silly, Miss Tushy na Let’s Bang the Babysitter miongoni mwa nyinginezo 120.
Kabla ya kuanza kutoka kimapenzi na afisa wa polisi aliyempa mtoto mnamo 2012, Kendra alikuwa hawara wa kuvua nguo katika vilabu vya starehe tangu 2008.
Alitumia fedha alizozipata kutokana na mauzo ya filamu zake kusomea shahada ya uuguzi kati ya 2009 na 2011.
0 Comments