Jane Wawira ambaye ni afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya kibinafsi ya usalama ya Trimo ni mmoja wa wanawake ambaye amethibitisha kuwa hakuna kazi iliyotengewa wanaume wala wanawake
Kando na kuwa na umbo la kuvutia, Wawira anajulikana nchini kwa kukabiliana na wahalifu wakubwa na kampuni yake imetambulika mara kadhaa kwa utendakazi wema.
TUKO.co.ke iliweza kubaini kuwa Wawira ambaye ni mama wa mtoto mmoja alipata mafunzo ya ujajusi katika idara ya upelelezi, CID.
Wawira ametuzwa humu nchini na idara ya polisi na hata kimataifa kwa kazi nzuri hasa ya kukabiliana na uhalifu.
Afisa huyo amewahi kukiri kupitia changamoto nyingi katika wadhifa wake na hata kufichua jinsi ametishiwa maisha na watu kadhaa.
0 Comments