KANGA NYEPESI INAVYOSISIMUA KATIKA MAPENZI

Kuna baadhi ya wanawake ambao wapo katika mahusiano hawajui umuhimu wa vazi la kanga nyepesi ambazo husaidi kuongeza msisimuko hasa unapokuwa chumbani na mpenzi wako.

Unapokuwa umefunga vazi hilo ambalo ni aina ya mtego huku ukiwa unajipitisha yaani unakuwa unampagawisha balaa.

Na kama unapika chakula au unafanya shughuli nyingine ukiwa katika hiyo kanga moja hakika humsisimua mwanaume wako.


Kuna uwezekano hata hicho chakula usimalize kukipika tayari mwanaume atakuwa kashakuomba mchezo kutokana na msisimuko alioupata.

Wengi hawajui umuhimu wa hiki kivazi walahi hata usingekuwa unapoteza muda wa kukimbizana na mchepuko wa mumeo embu angaika na hiki kivazi utanipa matokeo.

Hakikisha unapokuwa kwenye hicho kivazi usiwe umevaa chochote kuwa kama ulivyozaliwa alafu jipitishe huku unajifanya kama huna muda naye unajifanta unatafuta kitu ndani ya kabati mara umetoka.

Mwanaume hawezi kuvumilia huo mtego jifunze vitu vya kumvuta mpenzi wako lazima atake mchezo hata mara nne kwa siku hayo ndio matokeo ya kanga laini.

Yaani unaweza kumfanya mwanaume wako hata asitoke nje au akitoka anarudi fasta maana anakuwa anakuwazia jinsi alivyokuacha ndani ya kivazi laini anaona bora amalize kazi zake haraka aje kuburudika.

Jamani hata kufanya hivyo kunakushinda kweli mpaka mchepuko akusaidie ukiwa na mumeo chumbani usiogope kuvalia hicho kivazi.

Kuna baadhi ya wanawake wanatia aibu jamani upo na mumeo nguo alilovaa utasema anakwenda kuvuna mahindi shambani.

Tubadilike jamani hata matenge tuyaache kufunga hayana msisimuko yaani hata mwanaume hashtuki kukuona.

Vazi hili linasaidia kudumuisha mahusiano yenu na hata ndoa yako kudumu asiende kwa mchepuku.

Hivi kama unamfanyia mpenzi wako hiyo mitego ya chumbani unazani kwa mchepuko atakwenda kufuata nini wakati kwako kila kitu anakipata.

Pia ikiwa mnaishi peke yenu, siyo hatari hata kidogo kuvaa kanga moja, akazurura nayo sebuleni, jikoni na sehemu nyingine za nyumba yenu.

Nasema hivyo kwa sababu, kuvaa minguo kibao mbele ya mumeo naweza kusema ni ushamba, labda kama kuna baridi sana, unaumwa au hauko vizuri na mwenza wako.

Kinyume chake unaweza kuvaa vazi hilo na ikawa ni chachu ya mambo yetu yalee.

Wanaume wanatekwa na vitu vidogo sana jifunze mbinu mbalimbali za kummiliki mpenzi wako usikubali mchepuko akuzidi.

Shida inakuja pale utakapovaa vazi hilo kisha kutoka na kwenda bafuni kuoga nje, mbaya zaidi uwe umejaaliwa umbile tata kama langu kisha kwenye nyumba unayoishi kuna wanaume kibao.

Unadhani katika mazingira hayo ndoa yako itakuwa salama kweli? Unadhani wapangaji wenzako watakuheshimu? Sidhani kama itakuwa hivyo.

Hili vazi unalivaa mkiwa chumbani sio unaenda nayo hadi mtaa wa pili huko utakuwa unatafuta mambo mengine.

Post a Comment

0 Comments