KAMPUNI YA URUSI YAKOSOLEWA KUWALIPA WASICHANA WANAOVAA SKETI KATIKA KAMPUNI


Kampuni ya Urusi imekosolewa sana kwa kuwalipa wanawake pesa za ziada ili wavae sketi au gauni wawapo kazini.

Kampuni hiyo Tatprof, ambayo hutengeneza bidhaa za aluminiamu inaendesha kampeni ya "muonekano wa mwanamke " hadi tarehe 30 Juni.

Wafanyakazi wanawake wanaovaa sketi "ambazo zina urefu usiozidi sentimita tano juu ya magoti " yaani fupi wanalipwa dola $1.50, zaidi juu ya mshahara wao wa kawaida.

Ili kupata pesa hizo za ziada, wanawake wanatakiwa kutuma picha zao kwa kampuni hiyo.

Post a Comment

0 Comments