KUTANA NA MCHUMBA WA BETTY KYALO MWENYE ASILI YA KISOMALI

Mchumba wa Betty Kyallo amefichuliwa na mashabiki wake.

Huyu ndiye mwanamume aliyemchukua kupunga upepo pale Naivasha siku ambayo Dennis Okari alipokuwa anajishughulisha na bibi yake, Naomi Joy.

Mchumba wake wa siri sasa ametambuliwa kama Nasir alimchukua Betty mwishoni mwa wiki kujiburudisha kwa Enashipai Resort, Naivasha.

Ili kujenga msingi wa habari hizi, Betty Kyallo aliweka mfululizo wa video kwenye Instagramu zinazoonyesha yeye na mchumba wake wa siri.

“Nahisi kama msichana mchanga, enyewe nafeel poa sana, Blessings tu,” aliweka maandiko haya ikiandamana na picha.


Inaonekana sasa mchumba wake ni wa jamii ya Kisomalia na anaishi nchini Uingereza. Mapema mwaka huu, Betty alikuwa Uingereza akimtembelea.

Aliwaambia mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii, “Safiri maili milioni ili kuona tabasamu #SohoNights.”

Yeye sasa yuko Kenya na baadhi ya watu tuliozungumza nao wanasema  kwamba “anamchukua kutoka kazi na daima huonekana wote wanapendeza.”

Betty Kyallo anamiliki chumba cha mapambo cha ‘Flair by Betty’ kwenye sehemu ya kitajiri ya Kilimani na wengi wa mashabiki waliomwona walisema yeye huchukuliwa kazini na mchumba wake.

Alionekana kwenye kikao cha kusikiliza albamu ya Patoranking huko Kiza.

Kwa hisani ya buzzcentral.co.ke

Post a Comment

0 Comments