MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA ILI UWEZE KUDUMU NA MPENZI WAKO


Katika suala la ndoa kuna mambo mengi ambayo unatakiwa kuzingatia leo nitakupa mambo matatu ya kuzingatia ili mumeo ama mchumba wako akupende zaidi.

mapenzi ili yawe matamu basi mwanamke unatakiwa kuhakikisha jambo la kwanza unamuamini mume wako au mchumba wako.

Hilo ni jambo muhimu miomgoni mwa vitu vinavyovunja mahusiano ya watu wengi katika karne hii ni pamoja na kukoseana kwa neno uaminifu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Jambo hili limekuwa likiwakuta kwa asilimia kubwa wanawake, yaani utakuta mtu anamuliza mume wake upo wapi, hata mumewe akitaja sehemu sahihi aliyopo bado mwanamke huyo hata amini vile vile.

Lakini jambo la kushangaza mwanamke akidanganywa ndio anaamini inatakiwa ifike wakati ukiambiwa jambo na mpenzi wako basi ujitahidi kumuelewa.

Wanaume huwa hawapendi kutokuaminiwa yaani ni kitu ambacho kinawakera sana anapenda anapokujulisha jambo basi ukubaliane naye na sio kila wakati kumuhisia mambo mabaya.

Pia kuna wanawake wengine ni kero jamani hapa lazima tuambiane ukweli itakuta mwanaume kachelewa kutoka kazini alibanwa na kazi za ofisini karudi amechoka anafika nyumbani anapokelewa na maneno mzito ulikuwa kwa michepuko yako imekuchelewesha kurudi nyumbani.

Ukicheki muda ni saa nne usiku basi hilo neno la mchepuko anavyoliongea akienda kuoga analo akienda kula chakula analo akaji kulala analo. Unaona hata mapenzi hatufanyi kwa sababu mchepuko amekuchosha.

Embu jitahidini wanawake wenzangu kumuamini mume wako ama mchumba wako wanaume hawapendi kero hasa kama hawajachepuka alafu unamshikilia bango hilo yupo tayari kukuacha haijalishi amekuoa au la.

Hivi unadhani kila siku unamuambia mumeo anachepuka wakati hafanyi hivyo unafikiri nini kinafuata kama sio kutafuta mchepuko ili atulize nafasi yake.

Wanawake muache kuwatafutie wanaume zenu dhambi za kilazima sio vizuri kuweni wastaaramu katika mahusiano ukiamua kumpenda mtu jambo muhimu ni kutakiwa kumuamini.

Unapoweka uaminifu kwake hata kama anafanya ujinga atajitahidi kukuheshimu hawezi kukubali kukuumiza kwa sababu anajua wewe unamuamini kwa asilimia mia.

Pia kwa mwingine anaweza akaogopa hata kuchepuka akihofia uaminifu uliouweka kwake.

Jambo jingine wanawake mnatakiwa kushukuru kwa chochote ambacho amepewa na mumewe.

Utakuta mtu ameletewa zawadi na muwewe lakini kwa kuwa hajaipenda zawadi hiyo, utashangaa majibu ambayo yanamtoka kinywani mwa mwanamke huyo baadala ya kushukuru, utakuta mtu anasema ni kitu gani hiki ambacho umekileta? Na majibu mengine mengi kama hayo

Hata zawadi iwe nzuri au mbaya unatakiwa kushukuru na kumuambia muwe wangu asante kwa kile ambacho umeniletea ili kumridhisha mume au mchumba wako.

Post a Comment

0 Comments