JINSI AMBAVYO BI HARUSI ANAPASWA KUJITUNZA ILI AONEKANE AMEPENDEZA

Na MARGARET MAINA

KILA biarusi hutaka kung’aa siku ya harusi yake.

Tumekuwa tukishuhudia mabibi harusi wakitumia miezi kadhaa kupanga mambo mengi yahusianayo na siku ya siku.

Cha muhimu ni urembo wa miili yao.

Kuosha na kuipa unyevu ngozi ya uso

Ikiwa wewe ni biarusi mtarajiwa, anza matunzo ya ngozi yako ya uso kwa kufuata utaratibu wa kuosha, ku-tone na kuipa unyevu ngozi ya uso.

Unatakiwa kufanya hivi kila siku bila ya kuacha. Kufanya hivi kutasaidia kuifanya ngozi yako kung’aa.

Kusafisha uso kunasaidia kufungua matundu (pores) – yaani vinywelea – na kuifanya ngozi ipumue vizuri.

Ku-tone kunasaidia kufunga matundu na kuondoa uchafu uliosahaulika wakati wa kuosha.

Tunaipa ngozi unyevu kwa kutumia losheni ya uso ambayo pia inaipatia ngozi virutubisho na kuifanya ngozi kuwa laini na nyororo.

Ni vizuri zaidi ukitumia losheni yenye SPF (Sun Protecting Factor) ambayo itakusaidia kukulinda dhidi ya athari zinazotokana na miale ya jua.

Kuondoa ngozi/seli mfu

Hii ndiyo njia nzuri zaidi itakayokuwezesha kuwa na ngozi nzuri isiyo na seli mfu. Hakikisha unaondoa seli mfu kwenye ngozi yako ya uso kabla ya kutumia sabuni ya kuoshea uso.

Mbali na uso, sehemu za mwili zilizobakia pia zinatakiwa kufanyiwa kufanyiwa huduma hii (exfoliation). Fanya hivyo mara mbili mpaka mara tatu kwa wiki.

Unaweza kutumia scrub zilizotengenezwa nyumbani au zile ambazo tayari zimeshatengenezwa na zinapatikana madukani.

Mlo kamili

Unatakiwa kunywa maji ya kutosha ili kuondoa sumu mwilini. Kunywa angalau glasi 8 mpaka 10 za maji kila siku. Baadhi ya nyakati ni vizuri pia ukinywa maji ya dafu ndimu au limau.

Kula mlo kamili utakaojumuisha matunda, mboga za majani, protini.

Ni vizuri na ni muhimu sana kuupatia mwili anti-oxidants na madini ili uwe na afya nzuri na ngozi nzuri, yenye afya, kung’aa na kupendeza.

Ukosefu wa Vitamini na madini husababisha nywele kukatika na ngozi kupoteza mvuto na uzuri wake.

Mazoezi

Mazoezi nayo ni muhimu.

Kulala

Ni muhimu sana kupata usingizi wa kutosha hasa siku yako kuu itakapokuwa inabisha hodi. Kupata usingizi wa kutosha kutakusaidia au kutaondoa kabisa hatari ya kuwa na weusi kuzunguka eneo la macho.

Kisayansi tunashauriwa kulala angalau muda wa saa kuanzia nane hadi 10 kila siku.

Tahajudi (Meditation)

Ni moja kati ya njia nzuri zaidi ya kupunguza stress. Jipe muda binafsi, meditate kwa angalau dakika 15 kwa siku.

Jitahidi kufikiria mambo mazuri yaliyopo, mazuri yanayotarajiwa kutokea karibuni, fikiria mazuri zaidi yatakayotokea baada ya harusi.

Utatawaliwa na amani ya nafsi na furaha muda wote.

Furaha hii inafaa kuwa ilianza jana, ipo leo, siku ya harusi na itaendelea hata baada ya harusi.

Post a Comment

0 Comments