Haya ndiyo mambo matano (5) unayopaswa kujiambia mwenyewe kila siku

Related image

Katika kitu ambacho kitakuwa na thamani kubwa katika maisha yako, ni vile amabavyo utakuwa na uwezo wa kujinenea mambo chanya kila wakati. Kwani watu wengi wamekuwa hawafanikiwi kwa sababu wamekuwa ni watu ambao wanajikatisha tamaa wao wenyewe.

Hivyo ili kuondokana na thana hiyo haya ndiyo mambo ambayo unatakiwa kujiambia mwenyewe mara kwa mara kila uianzapo siku yako.

1. Leo ni siku yangu ya kuweza kufanikiwa kwa kutenda kile nilichokuwa nimekipanga jana.

2. Mimi ni  bora hakuna wa kunikatisha tamaa, kwani hatima ya maisha yangu ninayo mwenyewe.

3. Kwa haya nitakayotenda leo naamini mimi nitakuwa mshindi, kwani yatakwenda kubadilisha historia ya maisha yangu.

4. Mimi naweza, na nitafanya kwa ubora jambo hili, kwani  hakuna wa kunizua kuyapata mafanikio yangu.

5. Kwa hayo yote naamini ya kwamba mwenyezi Mungu atakuwa nami katika kunisimamia hayo yote ambayo nitayatenda siku ya leo.

Hayo ni baadhi ya maneno amabyo unapaswa kujiambia kila wakati na kila siku unapoianza siku yako ya mapambano dhidi ya kuuaga umaskini.

Na ili hayo yote yakamilike unahitaji kuamini na kuwa chanya kila wakati.

Na. Benson Chonya

Post a Comment

0 Comments