Chuki Dhidi ya Wapenzi wa Jinsia Moja yawa Kosa la Jinai

Related image

BRAZIL:Majaji wa Mahakama ya Juu nchini humo wamepiga kura iliyotoa uamuzi huo. Kura 8 kati ya 11 zimepitisha kuwa chuki dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja kuwa kosa la jinai

Mtu atakayetenda kosa hilo la chuki atashtakiwa sawa sawa na mtu aliyetenda makosa la ubaguzi wa rangi

Hata hivyo uamuzi huu utasubiri sheria ipitishwe na Bunge ambalo linatajwa kuwa na Wabunge wengi wahafidhina na waumini wa Makanisa ya Kiinjili

Takwimu zinaonesha kuwa nchini Brazil watu 358 waliuawa kwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja katika miaka 40 iliyopita huku 58 wakijiua mwaka 2017 

Post a Comment

0 Comments