HAITHAM KIM: AMBER LULU NI MWIZI, KINYANG'ANYI

Me namwitaga nyaku nyaku!

Aliaanza kwa kuongea hivyo msanii wa mzuki wa kizazi kipya nchini na video vixen Haitham Kim akifunguka juu ya msanii mwenzake Amber Lulu akimshutumu kujaribu kumuibia mume wake.


Mapema mwezi wa tatu mwaka huu wawili hao waliingia katika bifu kubwa baada ya Haitham Kim kumtuhumu Amber Lulu kwa kutaka kumuibia mume wake,Wadau wengi waliamini kuwa ilikua ni kiki.

Iliaminika ni kiki kwakuwa wawili hao washawahi fanya kazi pamoja iitwayo Kigogo na kuwa wawili hao wana song jipya linakuja.


Akizungumza na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv Haitham Kim baada ya kuulizwa kama wameshasamehana msanii huyo amedai kuwa msanii huyo mwenzake ana tabia mbaya.

Na pendaga kumuita kidudumtu..kinapenda sana kuingilia maisha ya watu… anatakiwa kutengeneza na sio kufatilia mabwana za watu

Ameendelea kudai kuwa Amba Lulu hana historia nzuri na mabwana za watu.

Ukisikia huyu ni mwanamume wangu ujue kamuiba kwa rafiki au ukisikia ni mume ujue kamuiba kwa mtu.

Haitham Kim ameendelea kudai kuwa walishayamaliza yeye na mumewake na alikuja kugundua kuwa haikua kweli kuwa mumewe anatoka na Amber Lulu na kudai kuwa ni Amber Lulu ndiye alikua ana-inittiate hali hiyo.

Cheki interview kamili aliyoifanya na Wasafi Tv hapa chini…

Pia kwasasa ametoa kibao kipya kwa jina la ‘Pasikona’ yenye maadhi fulani ya mduara hivi ,enjoy hapa chini..

Post a Comment

0 Comments