Uyu binti nibinti nilitokeaga kumpenda sana tena sana miaka 3 nyuma (wakati huo tupo kwenye mahusiano ya kufa tu)
Ni binti ambaye ansoma chuo kikuu kimojawapo hapa tz (anasomea udaktari )
Kipindi cha nyuma uyu binti nilimpenda ila hakuonekana kuja kabisa upendo wangu
Nakumbuka mwaka jana aliniambia N naomba mapenzi yetu yaishie hapa (niliumia mno mno ) na mpaka akaemtext dada yangu kuwa mimi na yeye mapenzi basi
Sikuwa na jinsi, mtoto wa kiume nikakaza moyo nikasonga mbele (nilifuta kila kitu Chase kwenye simu yangu)
Safari yangu ya kuendelea na harakati angu ikasonga mbele (wakati ananiacha, alijua kabisa mimi nimesomea computer )
Kama mwezi ukapita pasipo mawsiliano yeyote baina yetu wawili
Siku iyo nakumbuka baada ya mwezi alinipigia simu kuniomba nimsaidie kitu kwenye computer yake maana alisema inasumbua, nilimuelekeza kwa njia ya simu aende kwa mafundi pale machinga complex (uyo fundi no rafiki yangu) maana sikuwepo dsm
Alifanya ivyo na alifanikiwa, mawasiliano yakaishia hapo hapo
Sasa siku zikasonga issue nyingine ikaja kuwa ivi
Miezi 5 nyuma uyu binti alipoteza simu alinipigia, akanipigia usiku (saa 4) kwa namba ngeni kabisa akaniambia alikuwa ana tatizo kwenye pc yake nimsaidie nikamuambia mbona namba ngeni ( namba yake ilikuwa ni 07, so nikishangaa kuona siku iyo ni 06)
Akaniambia kuwa amepoteza simu ina karibia siku ya 4, nikamuambia umeenda polisi akasema yeah amefanya ivyo
Nikamuaomba anipe kadhaa, simu yake ataipata (alicheka na kuona kuwa nmfanyia mzaa)
Nilimsaidia tatizo lake aliloitaji kwa siku Ile kuhusu computer yake, basi bwana mtu mzima nikaingia chimbo kuitafuta simu yake, kuna rafiki yangu yupo kitengo cha usalama wa mitandao nitamfikishia ombi langu, akanisaidia nashukuru ndani ya week moja simu ilipatikana kupitia kwa mtuumiwa aliyekutwa nayo
Baada ya mtuumiwa kupatikana nilimpigia Yule demu aje nilipo alisema yupo busy kidogo maana alijua namuita kwa mambo yangu binafsi
Ikabidi apigiwe simu na askari wa pale kituoni, ikabidi aje mpaka pale, alikuwa anaogopa sana maana akujuelewa nini ninaendelea
Basi alipofika aliojiwa na akakabidhiwa simu yake na issue iliishia pale
Tukaondoka wote mimi na yeye
Tangu siku iyo nikiri mbele za mungu uyu binti amekuwa akinijali kwenye kila hali amekuwa akionyesha ukaribu mkubwa sana na mimi kupita kipidndi kingine chochote,
Yaani mpaka mimi ananiogopesha wadau, kwa siku lazima anipigie simu si chini ya mara 4
Ndio ivyo, je wadau hii hali inatokana na nini
Je ni maigizo ya uyu binti au nini
Maana mara kwa mara umtafuta dada yangu na kuongea nae pia
0 Comments