HALIMA Yahya ‘Davina’ ameonesha kufuata nyayo za staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Mondi’ kwa kuanzisha ‘brandi’ yake ya pafyumu. Mrembo huyo kutoka Bongo Movies ameliambia Amani kuwa, malengo yake makubwa ni kuhakikisha anafanya vizuri kwenye eneo la ujasiriamali kwani anaamini huwezi
kufanikiwa kama atategemea chanzo kimoja cha mapato. “Sanaa pekee haitoshi, nimekuja na pafyumu na losheni na kama unavyojua pia nina kampuni yangu ya kupika chakula, sishindani na mtu bali nafanya mambo yangu kuhakikisha tu ninakuwa na vyanzo vingi vya mapato,” alisema Davina. Mbali na Diamond, mastaa wengi kwa sasa wamejikita kwenye ujasiriamali kama huo akiwemo staa wa Bongo Fleva, Hamisi Mwinjuma ‘MwanaFA’.
0 Comments