Grace mwenye umri wa miaka 21, ni mwanadada ambaye amepitia majaribio aina mengi duniani licha ya umri wake mdogo.
Akisimulia kisa chake kwa mtangazaji Massawe Japanni, Grace alisema kuwa aliolewa akiwa na umri wa miaka 19 pindi tu alipokamilisha masomo yake ya shule ya upili.
Grace anadai kuwa alikuwa na urafiki na jamaa fulani na walipoanzisha uhusiano, alipachikwa mimba na kama ilivyo desturi ya ndoa za watu wachanga, yule jamaa alimuahidi kuwa atamuoa.
Mwanadada huyu alitoroka kwao na kwenda kuishi na mpenziwe huku asijue kilichokuwa kinamngoja.
Anadai kuwa alipokaribia kujifungua, mpenziwe alianza madharau madogo kama kule wanawake wengine nyumbani kwao na isitoshe alikuwa anampa kichapo cha mbwa bila sababu.
Grace aliongeza kuwa pindi tu alipojifungua, mpenziwe alikuwa anamuamrisha afanye kazi ngumu ngumu hadi usiku wa manane bila huruma.
Alidai kuwa alipotoka nyumbani kwao wazazi wake hawakufurahishwa na hatua yake, na basi ilimbidi kutafuta usaidizi kwa ndugu zake ambao walimuekea biashara.
Kuona vile, mpenziwe alipatwa na wivu na alizidi kumpiga akidai kuwa anachekesha wateja wake badala ya kufanya kazi.
Hapo ilimbidi aondoke na kwenda kwa nyanyake bila hata kubeba mavazi yake au ya mtoto wake ili kuondokea masaibu hayo yote.
Soma usimulizi wake.
Mimi nilikuwa shule na nilipomaliza form four nikapatana na kijana akanipachika mimba na a aliniahidi atanioa, nikatoroka nyumbani na nikaenda kuishi naye.
Nikiwa nimebakisha wiki mbili nijifungue akaniletea mwanamke mwingine kwa nyumba na akanipiga hadi nikavunjika mgongo, saa hizo nilikuwa na miaka 19.
Niliteseka lakini nikaamua kuvumilia kwani nyumbani niliambia niliambiwa kama sitaki kusoma basi niishi na yule kijana.
Alianza kunionyesha madharau anaenda analala nje anarudi asubuhi, bahati nzuri nikazungumza na ndugu zangu na wakanifungulia biashara.
Nikifanya biashara kumbe hakuwa anafurahia na nikipeleka chakula kwa mafundi kumbe ananichungulia kwa dirisha. Nikicheka anakuja kwa nyumba kuniuliza nacheka nini na ananichapa.
Mpaka nikaamua kunywa sumu lakini mama mwingine akaja akaniongelesha na nikatoka bila hata nguo za mtoto sahii naishi kwa nyanyangu.
0 Comments