Tabia ya Shamsa Kutopenda Wageni Wakati wa Kula

MSANII wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford amefunua siri ambayo watu wengi walikuwa hawaijui kwamba enzi za utoto wake alikuwa hapendi wageni wafike nyumbani kwao wakati wa kula kwa sababu alikuwa anaona watawamalizia chakula chao.



Akizungumza na Ijumaa Wikienda msanii huyo alisema kuwa, alikuwa hapendi kabisa hayo mambo ya wageni kwenda nyumbani kwao wakati wa chakula, kwa kuhofia kuwa watamaliza chakula chao, hali iliyopelekea kupigwa na mama yake kila siku kwa ajili ya tabia yake hiyo mbaya.



“Nakumbuka enzi za utoto wangu nilikuwa sipendi wageni kabisa hasa linapokuja suala la kula, yaani nilikuwa naona kama wakija watatumalizia chakula, hivyo hali hiyo mama yangu alikuwa haipendi, alikuwa ananipiga kila siku, nikikumbuka acha tu kwani nimechapwa sana, hata hivyo sasa nashukuru Mungu hiyo tabia ilikuja kuisha,” alisema Shamsa. 

Post a Comment

0 Comments