Ule upendo Wa zamani baina ya mtu na mtu, rafiki na rafiki, jirani na jirani hata jamaa kwa jamaa haupo tena!
Siku hizi hata marafiki Wa damu wanaoneana wivu na husda, Machoni wanachekeana lakini moyoni hawatakiani heri!
mfano;
Unakuta mtu na jamaa yake ni marafiki kabisa lakini mmoja akijenga nyumba nzuri zaidi ya wenzake; marafiki zake wanakata mguuu, Wanaacha kumtembelea hata akiwaalika hawaji (wivu)
Hata rafiki akinunua Gari zuri baadhi ya marafiki wanajitenga nae!
Siku hizi ujamaa umeondoka kabisa watu wamekuwa na roho mbaya na wivu wenye husda!
Wazee wetu hawakuwa hivi, kwanini kizazi chetu kimekuwa kizazi cha kuoneana wivu? nini chanzo? Je ni ukosefu Wa ajira au ni ongezeko la mianya ya rushwa linaloibua matabaka?
Toa maoni yako!
0 Comments