Kajala Amkumbusha Lulu ya Segerea

STAA wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja baada ya kumtakia heri ya kuzaliwa muigizaji mwenziye Elizabeth Michael ‘Lulu’ alimkumbushia mambo ya gerezani Segerea kipindi walipokuwa na misala.



Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Kajala alisema sababu ya kumkumbushia mambo ya Segerea ni kutokana na furaha aliyokuwa nayo kwani alikumbuka msoto waliopitia pamoja walipokuwa huko.



“Nilimkumbusha Lulu kuhusu vibarua tulivyokuwa tukifundishana jinsi ya kuviandika tulivyokuwa mle ndani, nilifurahi maana kumbukumbu nyingine zinaweza kukufanya ukacheka au ukalia kabisa, watu tumepitia magumu na tumetoka mbali,” alisema Kajala. 

Post a Comment

0 Comments