Muigizaji Mwijaku aeleza utajiri wake



Mwigizaji wa tamthilia, Mwijaku amewafungukia wale wanaomchukulia poa kwenye mitandao ya kijamii na kuwaambia kuwa kimaisha hawalingani na yeye.

Pia amesema hatoacha kuongea na kuwakemea vijana wanaotupia picha mbaya mitandaoni kwani anataka wakae kwenye mstari mzuri kimaadili.

"Kuna watu wananichukulia poa, kimaisha nalingana na wazazi wao,najenga maeneo ya Mpinga nina mashamba Bunju na  Bagamoyo, nina magari nane, nimiliki ‘Ubber’ nne, yote kwa sababu ya kuigiza kule kupost ‘Instagram’ ni kuongea kuwakumbusha vijana wenzangu wanaojisahau," amesema.

Ameendelea kwa kusema, 'Kuna wengine wanapiga picha mbaya siwezi kuwaacha lazima niwaambie kwa sababu nawatakia mema’.

    

Post a Comment

0 Comments