Wanawake Tuache Tabia ya Kuwaachia kila kazi Wafanyakazi wa Ndani..Mtasaidiwa Mpaka Kitandani..Soma Kisa Hichi

MUME: Darling nina kikao mkoani kesho naomba niandalie vitu please.
MKE: Dada zile nguo za baba pamoja na soksi ulifua.
DADA:Ndio nimepanga kabatini. mama anarudi chumbani na kumuomba hubby wakacheki TV sebulen, lakini baada ya muda mama anamuita dada akapange suruali kadhaa na mashati kwa ajili ya safari ya kesho, dada anapanga kila kitu anatoka



MKE: Kama tayari hakikisha unarekebisha yale mashuka pale kitandan weka na maji bafuni, dada anafanya na kwenda zake kulala, asubuhi dada anaamka mapema na kuandaa kila kitu ikiwamo na chai, baba anakunywa chai na kutaka kuondoka.

MKE: Dada msindikize baba ili ufunge geti sbb bado ni giza.

DADA: Sawa mama, dada anatoka na begi la baba hadi nje kwavile mkewe yupo ndani , baba anamtaka dada abaki vizuri na watoto, dada anaitika na kusema nawao wanamuombea safari njema. Baada ya muda baba anarudi toka safari

MKE: Huku akitabasamu, dada si umemuona baba amerudi vipi chakula tayari.

DADA: Ndio.

MKE: Haya kapange meza vizuri mimi nandaa juice. Baada ya muda wanakula na baba anagundua juice sio nzuri anaamua kuiacha na kusema leo wamesahau kuweka baadhi ya vitu hivyo hataweza kuinywa.

Baadae baba anakumbuka kuwa aliacha boxer zake kwenye ndoo ya maji chumban na kufunika mfuniko, anamuuliza mama vipi zile nguo zangu kwenye ndoo zilifuliwa maana nilisahau kusema kama zina maji.

MKe: Dada njoo hapa hivi zile nguo za baba chumbani ulifua.

DADA: Ndio mama lakini hasemi kama alianua na kuweka chumbani kwake akidhan atakunja baada ya kazi kupungua
MKE: Darling zilifuliwa.

MUME: Na watoto vipi wameshalala.
MKE: Anajibu wamelala darling.

MUME: vipi dereva wao alifika kuchukua pesa yake.

MKE:Dada eti uncle Hassan amechukua pesa yake.

DADA:Hapana wamembadilishia gari uncle Hassan amesafiri kwa muda.

MKE:Tutampatia darling siku akirudi acha dada aendelee kuitunza.

MUME: Basi vizuri, ehee vipi na tution walienda leo.

MKE: Ndio walienda anamgeukia dada, si eti ee walienda si eti.

DADA:Hapana Kelvin anaumwa leo siku ya pili nilinunua dawa dukan nimempa lkn hajambo

MKE:Anashangaa hee mtoto mgumu huyu kumbe jana alikua mgonjwa halafu wala!!! alikua anacheza tu jamani watoto,asante dada umefanya vizuri.

MUME: Haya mimi niwaache nataka nikapumzike lkn darl nitaomba zile boxer nichome kabla ya kulala sababu zimeanza kuchoka

MKE: Anaingia chumbani anafungua kabati na kuzikosa lkn kabla hajajieleza anamuona dada analeta mzigo wa boxer zikiwemo chupi za mama na mataulo.

MUME: Basi dada zirudishe tutachambua kesho nenda kafanye kazi zako, mume anainuka na kuelekea kulala, lakini anagundua mke wake alimwaga nguo kitandani wakati anatafuta boxer hivyo anaamua kurudi sebuleni ili aombe. kuandaliwa kitanda, kwavile chumba cha dada kipo jiran na chao anagundua dada ameacha mlango wazi.

Anaamua kuufunga ili mbu wasiingie lakini anaona baadhi ya mashati na suruali zake zikiwa zimenyooshwa na kuwekwa pemben huku kitanda kikiwa kimetandikwa kwa ustadi anaamua kufunga mlango na kutoka, anafika sebuleni anakuta mama anatazama tamthilia anamwambia akatandike kitanda.

MKE: Dada njoo, (kwa sauti ya kunong'ona) naomba ukatandike kitanda haraka.

DADA:Tayari nilipeleka viatu vya baba nikaamua kutoa na zile nguo.

MKE: anaamka na kwenda kuhakikisha anarudi na kumwambia mumewe tayari aende akalale

MUME: anaenda kulala lkn huku akijuiliza sana ni nini amfanyie huyu dada kwa ukarimu anaowafanyia hapo nyumban, kwanza anajua ni vitu gani baba anabeba akiwa safarini, ndio pekee anaemtakia safari njema na kumuombea, ndio anaefua boxer zake na kutunza vizuri, ndio anaepika chakula kitamu, ndio anaetandika kitanda chake, ndio anaejua juice gani baba anapenda, ndio anaejua kama watoto wamerudi vipi kutoka shule, vilevile ndio anaejua kama watoto wake wanaumwa ama vipi.

Sasa mnafikiri baba atamzawadia nini huyu binti ambae amebakiza kujua style anazopenda baba tu, si atamfundisha ili kesho asimsumbue tena mke wake ambae kila kitu lzm amuulize dada.

Akina baba hawaridhiki lakini wamama jitahidini hata kama mnamajukumu kiasi gani.

Post a Comment

0 Comments