Utamu Usioisha Hamu – 6


 ILIPOISHIA IJUMAA…
“Madenge nina hamu sana leo, mkeo kama hayupo njoo mara moja chumbani kwangu, nimezidiwa sana please…”
“Mmh! Chumbani kwako siwezi kuja naogopa, unajua jamaa yako anakujaga bila taarifa, akinikuta… Sitaki vurugu…”
SASA ENDELEA…

“Njoo chumbani kwangu utajua, nimeacha mlango wazi…”
“Hawa majirani hawawezi kuniona..?”
“Mama Ashura amekwenda sokoni, huyo ndiye mmbeya wa nyumba hii, halafu jifanye unafagia hapo nje… Halafu ingia fasta…”
“Nakuja Madenge, ila mkeo je, hawezi kuja?”

“Hawezi, nimemsafirisha kwenda kwao na nimehakikisha amepanda basi la Tabora…”
“Sawa, leo nataka unipe hadi nilie kabisa machozi…”
“Madenge habahatishi, mke wangu mwenyewe huwa anaomba pooo…”

“Sawa, nakuja…” Mwanaume alisoma meseji zote na kujikuta mwili mzima ukimtoka jasho, hakujua Madenge anakaa chumba gani kwenye nyumba hiyo, alichoelewa ni kwamba demu wake yupo kwa mwanaume ndani ya nyumba hiyo ya kupanga. Kwa sababu hamjui Madenge mwenyewe, alitoka nje kabisa na kukutana na mama Ashura akiwa ametoka sokoni, alibeba kikapu cha ndizi.

“Shemeji habari…”
“Salama shem wangu…”
“Hivi Madenge anakaa chumba gani humu ndani shem? Nina mzigo wake…”
“Madenge anakaa chumba cha pili kutoka kwako, jirani yako hujui anapoishi…
Sijui kama yupo maana alimsindikiza mkewe Ubungo…

Sijui kama amerudi…”
“Ameniambia amerudi…” Mume wa Monica alidanganya.
“Basi, chumba hicho hapo… Gonga atatoka kama yupo…”
Mama Ashura alisema, hakujua kinachoendelea.

Mwanaume alitembea kwa hasira aking’ata meno. Alipofika mlangoni akasikilizia kwa sikio lake la kushoto, akasikia Samira wake akigugumia katika ulimwengu wa raha, hofu ikamuingia na kuhisi kizunguzungu cha ghafla, lakini alijikaza kiume na kujiambia…
“Unapaswa kuwa imara… Wewe siyo wa kwanza kufumania,” alipojiambia hivyo aliegemea ukutani, mama Ashura alipomuona akashangaa na kujiuliza kulikoni?

“Shem gonga mlango, labda amelala…”
“Hajalala,” alitikisa kichwa, akasikia kitu ambacho kilimchosha zaidi mwili na roho.
“Madenge unajua hii mimba ni yako… Wala siyo ya mume wangu aliyenipangishia chumba…”
“Sawa, sasa utafanyaje?”
“Mi’ nataka nikaitoe kabla haijawa kubwa…”

“Hapana, usitoe mtoto wangu, mpe mwenye kulipia chumba…
Mimi nitatunza mtoto kwa siri, wakati baba wa bandia akiwajibika ipasavyo.”
“Sijazoea kudanganya Madenge, yaani mimba yako, halafu nimbebeshe mwanaume mwingine mzigo, mtoto akizaliwa ataitwa ubini wa nani?” Samira aliuliza.


“Ubini wa mwenye chumba, ila siri tunaijua sisi kuwa ni mwanangu. Sipendi kabisa utoe hiyo mimba tafadhali! Nakuomba sana Samira wangu, unajua mimba zetu huwa hazitolewi hovyo, ukitoa unakufa…”
“Sawa darling, nitazaa kwa ajili yako…”
“Hayo ndiyo maneno, ndiyo maana nakupenda! Unajua kazi yangu ya kusukuma mkokoteni inanipa nguvu sana…”
“Una nguvu sana… Nimechimba dawa haraka…”

“Safi, mwanamke hupaswi kuchelewa kuchimba dawa, sasa tunakwenda raundi ya pili…”
“Ngoja nikaoge kwanza… Nimechoka!” Baada ya kusikia hivyo, mumewe Monica aliingiwa na ujasiri baada ya kusikia hata mimba aliyobeba Samira anayemtunza kwa kila kitu siyo damu yake. Aliondoka upesi na kutoka nje ya nyumba hiyo na kwenda dukani. Mama Ashura alishangaa mbona jamaa anakimbia hadi nje. Akacheka sana.

Samira alipotoka akamkuta mama Ashura anacheka, hakuelewa kinachomchekesha, mrembo huyo akaingia chumbani kwake chap! Hakujua kama mpenzi wake ameingia na kugundua kinachoendelea, alijifunga taulo na kuingia bafuni kuoga. Chumba chake kilikuwa na bafu ndani kwa ndani.
Dakika chache alisikia mtu akibisha hodi, akasema; “… ingia mlango upo waziii!”
“Nani?” Aliuliza Samira.


“Mimi…ninayekujali,” sauti ilimshtua sana Samira.
“Ohooo, mpenzi wangu… mume wangu…umekuja jamani…”
“Ndiyo mpenzi wangu, nimekumisi sana na hamu yangu ni penzi lako… Vipi mtoto wetu tumboni hajambo?” Jamaa alimuuliza kwa kumchora, Samira hakujua kila kitu kipo wazi, hakuna siri tena.
“Hajambo, amemmisi baba yake, anauliza umemletea zawadi gani?”
“Zawadi nzuri sana…”
Mwanaume alichomoa chupa kubwa ya bapa ya pombe kali na kuweka mezani, akamwangalia Samira huku akisema.


“Yaani mwanamke ana tamaa ya ngono huyu, kwa nini anisaliti..?” Aliwaza akachukua glasi ya pombe kali na kumimina nusu, Samira alitoka nje akamwacha mwanaume ndani. Alikwenda chumbani kwa Madenge.
“Usije mume wangu amekuja, sijui mijitu mingine inatokea wapi, hajanipa hata taarifa…”
“Kwani anakupaga taarifa akija huyo, basi nenda…” Madenge alisema. Wakati wakiagana, mama Ashura alisogea.
“Samira una hatari sana wewe, angalia ipo siku utauawa…”
“Na nini?”


“Sasa kwa Madenge ulikwenda kufanya nini?”
“Kwani mwanamke akiingia chumba cha mwanaume anafanya nini? Naomba usinifuatilie bibie…”
“Sawa, ila shauri yako, wanaume siyo wajinga kama unavyodhani. Anaweza akajua unamsaliti na kukukaushia,” mama Ashura alisema hivyo baada ya kuona mwanaume aliyempangia hajakasirika wala kuzozana, wanaongea na kucheka tu. Akashangaa sana.
“Huyu mwanaume hatari, kamfumania mkewe sasa wanacheka! Mbona pambe?” Alisema mama Ashura.

Post a Comment

0 Comments