Mambo Yanayochangia Mume Kutembea na Hausigeli



Ndugu zangu, malalamiko ya baadhi ya mabinti wanaofanya kazi za ndani ‘mahausigeli’ kuwazidi kete baadhi ya wanawake kwa kuwachukulia waume zao yamekuwa yakiripotiwa kila mara.
Si ajabu hata wewe unayesoma makala haya aidha umeshawahi kumsikia rafiki kama siyo jirani yako akikorofishana na hausigeli wake au kushuhudia hausigeli akifumaniwa na bosi wake.

Hakika ni matukio ya aibu sana. Inafika wakati unajiuliza inakuwaje mume anamtongoza na hatimaye kutembea na hausigeli wake? Ameshawishiwa na kitu gani au amekosa nini kwa mkewe mpaka anafikia uamuzi huo?

Kimsingi linapotokea tukio kama hili, wengi hujiuliza maswali mengi sana na majibu yake huwa ni magumu kupatikana. Hii ni kwa sababu ni jambo lisilotarajiwa kufanywa na mtu aliyestaarabika. Hata hivyo, tuna kila sababu ya kujua chanzo cha tatizo hili.

Nitajaribu kuzungumzia kipengele kimoja baada ya kingine kuhusiana na yapi yanayotajwa kuwasukuma baadhi ya wanaume kutembea na mahausigeli wao.
Wanawake wanajitakia

Ni jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa sana na baadhi ya watu kuwa, inakuwaje hausigeli anapewa majukumu ya kumhudumia mume wakati mke yupo?

Ni ukweli usiofichika kwamba, kuna baadhi ya wanawake ni malimbukeni wasiojua jinsi ya kuitunza ndoa. Hawajui namna ya kumshika mume na kumuepusha na vishawishi vinavyoweza kumfanya akamsaliti.

Ndugu zangu, kitendo cha mke kumruhusu hausigeli amfulie mumewe nguo zake za ndani, amuandalie chakula, ampelekee maji ya kuoga na mambo mengine kama hayo ndivyo vimekuwa vikichochea usaliti huu.

Kama mke hataki kusalitiwa kirahisi basi ajitahidi sana kuchukua jukumu la kufanya yale ambayo kwa kiasi kikubwa yakifanywa na hausigeli huweza kujenga ukaribu wa kimapenzi kwa mumewe. Kamwe usibweteke, ukibweteka hausigeli wako atakupindua na itakuwa ni aibu kwako.
Mahausigeli micharuko

Hivi inaingiaje akilini mke kuridhia kumuajiri hausigeli ambaye kwa macho tu anaonekana hajatulia? Unamuajiri hausigeli ambaye siku ya kwanza tu anataka umpe sehemu ya mshahara wake akafanye ‘shopping’ halafu unakubali, unajitaka kweli?

Post a Comment

0 Comments