HASIRA: CHANZO KIKUBWA CHA KUVUNJIKA MAHUSIANO MENGI


LAITI kama kwenye dunia hii kila mmoja angejitambua, akafuata misingi sahihi ya uhusiano, basi kusingekuwa na ugomvi.  Watu wangekuwa wanapishana tu kwenye mambo madogomadogo na kuwekana sawa kisha maisha yanaendelea, lakini kutokana na ugumu wa mioyo yetu, tunaifanya dunia kuwa uwanja wa mapambano. Watu wanagombana kila kukicha, wanapigana na hata kuuana, kisa mapenzi.
Ukifuatilia, chanzo kikuu cha matatizo haya huwa ni usaliti. Tamaa zinawatesa watu, wanashindwa kuishi njia kuu na kujikuta wakisababisha machafuko pindi watu wao wanaposhtukia mchezo huo.
Wengine hata siyo tamaa ya kitu au vitu, bali ni tabia tu. Hata ufanyeje ndivyo mtu alivyo tu. Yeye hawezi kutulia. Anataka huku, anataka kule; yaani ili mradi tu aufurahishe moyo wake kwa njia hiyo. Ukiachana na hayo, kipo chanzo kingine kikubwa cha machafuko ambacho ndicho nataka kukizungumzia leo. Chanzo hicho ni hasira. Hakuna asiyejua kwamba hasira ni hasara. Ukiziendekeza hasira siku zote huwezi kufanikiwa.

Post a Comment

0 Comments