MWANAUME, USIMWACHIE CHUMBANI HELA YA MATUMIZI MKEO

*MWANAUME USIMWACHIE MKEO HELA CHUMBANI*
MWACHIE MBELE YA WATOTO NA UMWAMBIE
NA MATUMIZI YAKE, NA WATOTO WASIKIE USIJE KUISHI MAISHA YA UPWEKE UZEENI
*MWANAUME*
Unamwachia mkeo hela ya Chakula Chumbani,
Mke Anatoka na Kapu anaenda kununua Chakula,
Anapika, Anawaambia watoto, Njooni Wanangu
Mle Nimewapikia Chakula Kitamu, Watoto
wakishakula Wanasema Asante Mama.
*MWANAUME*
Unamwachia Mkeo hela ya Nguo za Sikukuu
Chumbani,
Kesho Yake mkeo Anatoka kwenda Kununua
Nguo, Akirudi Anawaambia Wanangu
Nimewanunulia Nguo za Sikukuu Njooni Mjipimie,
Watoto Wakishajipima, Anawaambia Wanangu
Mmependeza Eeee, Simnaona Ninavyowapenda
Watoto wanafurahi na Kusema Asante Mama,
*MWANAUME*
Kila Aina ya Pesa ya Matumizi Unamwachia
Mkeo Hela Chumbani,
*MWANANUME*
Ukifika muda wa kutoa Ada Unamkabidhi Mkeo
Hela Chumbani,
Kesho yake Mkeo Anawaambia Watoto kuwa
Anaenda kuwalipia Ada ya Shule, Akirudi
Anawaambia Wananhu nimeshawalipia Ada, Na
gari za Shule Zitakua Zinawapitia, Nataka Msome
Wanangu ili Baadae Mje Mnitunze, Watoto
Wanasema Asante Mama.
*KIBAYA ZAIDI*
Ukifika muda wa kutoa Adhabu, Mkeo yeye hatoi
Adhabu, Anawaambia Watoto, Ngoja Babayenu
Arudi, Nawewe Ukirudi Unaelezwa na Mkeo
matatizo ya Wanao, Unachukua Bakora
Unawaadhibu Watoto, Bila kujua kuwa Unazidi
Kujenga Uhusiano M'BAYA na Wanao.
*NGUMU KUMEZA*
Ukifika Uzeeni, Watoto wako Hawana
*KUMBUKUMBU* Yoyote Ya mema uliowafanyia.
*MWANAUME KUWA MAKINI SANA*
*_ZINGATIA HAYO KWA MAISHA YA UZEENI_*
Najua wazee wenzangu mtakuwa mmenufaika na
somo hili....#JUMAPILI NJEMA MUNGU AWATANGULIE NA MAPUMZIKO MEMA

Post a Comment

0 Comments