HARMONIZE SASA ATAKA MTOTO KWA SARA


MKALI wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’, sasa yupo tayari kuitwa baba. Harmonize au Harmo anayekimbiza na Wimbo wa Uno amemwambia mwandani wake, Sarah Michelotti kwamba, kwa sasa anataka watoto wakati wa bethidei ya mrembo huyo mapema wiki hii.

“Nakutakia maisha marefu, nakupenda mke wangu, mwanamke wa chuma, nimekupata kwa ajili ya maisha yangu, nipo tayari sasa nataka watoto,” Harmo alimwandikia ujumbe huo Sarah.

Sarah ambaye ni raia wa Italia amekuwa kwenye mapenzi mazito na Harmo ambapo naye alijibu kimahaba;“Asante mpenzi wangu, mume wangu, nakupenda zaidi na zaidi, natamani mapenzi haya yadumu milele na milele katika maisha yetu.”

Post a Comment

0 Comments