Karibuni kwenye darasa letu la mahusiano bila shaka week end yako umeimaliza salama.
Siku ya leo utajifunza umuhimu wa kupendwa na sio kulazimisha kupendwa katika mahusiano achaneni na mapenzi ya kuigiza kwani mwisho wake sio nzuri.
Kuna mambo muhimu ambayo wanawake wenzangu tunapaswa kuyaangalia hasa tunapokuwa katika mahusiano.
Jambo la kwanza usilazimishe mwanaume akupende muache akupende mwenyewe.
Huwezi hata siku moja ukalazimisha kupendwa kuna vitu unaweza kulazimisha lakini si kupenda. Hapa tunatakiwa kuwa makini la sivyo madhara yake ni makubwa kwa baadaye.
Wengi wao hawajui nakuchukulia ni jambo la kawaida hakuna kitu kibaya kama kulazimishwa kupendwa utakuta mwanamke anamlazimisha mwanaume wake amuweke stutas ama profile ili kuonyesha kama kweli anakupenda.
Hivi utawekwaje Stutas wakati kiuhalisia hakuna kupendwa hata hizi hesabu ndogo ndogo za mapenzi unahitaji mkaguzi wa hesabu akusaidie kufanya uhakiki? Embu jiongeze
Naomba nikuambie hicho sio kipimo cha kukupenda mtu anayekupenda utamjua kwa matendo yake na wala sio kuwekana profile omba kupendwa akuweke moyoni achana na hayo ya stutas.
Mwanaume hashindwi kukuweka stutas kwa kuwa umelazimisha akuweka na anakuweka kwa kukuridhisha wewe lakini ukimuangalia moyoni mwake hana upendo na wewe.
Ukiona mwanaume wako hana upendo na wewe unaweza kuchapa mwendo mapema kwani unapolazimisha kuishi naye ipo siku moja atakuumiza.
Huenda akaenda kuoa mwingine wewe akakuacha haijalishi umezaa naye mtoto atakuacha kwa sababu wewe sio chaguo lake huku ukiambulia kupata maumivu,
Kuna wanawake wengine jamani sijui wanalogwa na nani eti anaona akimbebea mimba mwanaume wake ndio kupendwa ha ha ha hapo unatuanga maji kwenye kinu jua kuwa kama ameshindwa kukuweka moyoni hata umzalie watoto kumi hawezi kukupenda.
Tujitahidi kuwa makini katika hilo ndio maana utasikia mwanaume anasema wewe ndio ulilazimisha nikuoe kwanza sio chague lake. Kwa nini ulazimishe kuolewa acha mwanaume mwenye afanye hayo maamuzi.
Hakuna jambo gumu kama kulazimisha upendo embu tafakari na kuchukua hatua kuliko kuendelea kupoteza muda wako katika mahusiano.
0 Comments