Siku hizi wanaume wengi wanakumbana na shida ya kukosa uwezo wa kuwapa ujauzito wanawake wao. Sio kwa sababu hawana mapenzi ya kweli au hawana afya, ila kuna masuala fulani hayapo sawa. Kuna mambo kadhaa yanayosababisha kupunguza ufanisi wa mbegu za kiume na kuleta athari katika kutungisha mimba.
Kutokana na hali hii, ndiyo sababu wanaume wengi wakosa nguvu ya kuzalisha. Watafiti wamesema kwamba mtindo wa maisha kwa baadhi ya wanaume unaweza kuathiri ubora wa wingi wa uzalishaji wa mbegu za kiume.
Haya ndio mambo yanayosababisha matatizo mengi kwa wanaume kukosa nguvu ya kuzalisha kwa sasa.
1. Kuweka simu mara kwa mara kwenye mfuko wa mbele wa suruali. Tafiti zimeonesha kwamba kuna mionzi kwenye simu za mkononi ambazo zinaathiri kwa kiasi kikubwa nguvu za kiume na kushusha uwezo wa uzalishaji wa nguvu za kiume kwa asilimia 9.
2. Msongo wa mawazo. Mwanaume ambaye ana msongo mkubwa wa mawazo, kutokana pengine na kufanya kazi kupitiliza yuko hatarini sana kukumbwa na upungufu wa nguvu za kiume. Ufanisi katika vitu vingi ndan ya mwili hushuka ikiwemo uzalishaji wa nguvu za kiume. Tafiti zinaonesha kwamba mwanaume anayeishi kwa wasiwasi yuko hatarini kuwa na mbegu zisizo na ufanisi ambazo kimsingi hupoteza uwezzo wa kurutubisha yai.
3. Ulevi wa kupindukia. Unywaji wa pombe uliopitiliza ni adui mkubwa uzalisahi wa nguvu za kiume. Kimsingi, moja ya majarida ya masuala ya Afya lililochapishwa nchini England linaeleza kuwa unywaji wa pombe kwa angalau mara tano kwa wiki kunaathiri utengenezwaji wa nguvu za kiume na kusababisha shahawwa zisizo na afya.
4. Kuvuta Sigara kupita kiasi. Uvutaji wa sigara uliopitiliza una athari mbaya kwa ustawi wa nguvu za kiume. Hata hivyo, watafiti wanasema kwamba, mtu anapoacha uvutaji uliopitiliza kila kitu kinarejea katika utaratibu wake wa awali mwili, hivyo kurudisha ufanisi wa utengenezwaji wa nguvu za kiume.
5. Uzito mkubwa. Watafiti wanasema uzito mkubwa katika mwili wa mwanaume ni sabab kubwa pia ya kupungua kwa ufanisi katika uzalishaji wa mbegu za kiume. Hivyo wanaume wanashauriwa kudhibti uzito wao ili kuepukana na tatizo hilo.
6. Ukaaji wa muda mrefu katika mazingira ya joto. Inaelezwa kuwa kukaa muda mrefu katika maeneo yenye joto kali ni hatari kwa ustawi wa utengenezwaji madhubuti wa mbegu za kiume. Wataalam wanasema sehemu za siri za kiume hazitakiwi kuwekwa katika mazingira ya joto kupitiliza. Maana yake ni kwamba kuacha kuvaa nguo zinazobana sana katika maumbile ya kiume ili kujiweka katika tahadhari ya kuepukana na matatizo ya uzalishaji wa mbegu imara, hivyo kupungukiwa au kukosa kabisa nguvu za kiume.
0 Comments