DADA WA DIAMOND ATAFUTA MUME MITANDAONI

JESSCA NANANGAWE
DADA wa Diamond aitwaye Esma Platnumz amefunguka anatafuta mume wa kumuoa ambaye atakuwa amemzidi umri ili amzalie mtoto wa kiume.
Akizungumza na DIMBA,Esm, alisema, kwa sasa anatamani kupata mtoto wa kiume baada ya kuwa na wawili wa kike hivyo kupata mume kutamrahisishia kutimiza ndoto zake.

ìUkweli natamani kupata mwanaume wa kuzaa nae na kuendeleza familia yangu, sitaki mwanaume wa kunipenda mimi tu, nataka aipende familia yangu na kikubwa awe amenizidi umri alisema Esma.

Aidha mwanadada huyo alisema moja ya mipango yake kwa sasa ni kuwa na familia iliyotulia na kupata mume ambaye hatakua na skendo hasa kwenye mitandao ya kijamii.

Post a Comment

0 Comments