Mara sio moja umesikia msemo huu ‘ maisha ni mafupi’.Je ushawaji kujiuliza mbona binadamu hutaka maisha yawe marefemu ? Wengi wanajishughulisha na vingi ili kujiridhisha ,lakini hadi leo hakuna kitu ambacho huwapiga watu chenga kama mapenzi.Mapenzi humfanya hata mtu anayeonekana kuwa na uthabiti fulani au talanta au umaarufu kuonekana kama mtoto .Mapenzi yamefahamika kuwafanya hata walio na maamlala kuanzisha vita na taifa au ufalme jirani . Mapenzi yamefanya watu kuua . In short,Mapenzi yanarun dunia !
Lakini basi kama mapenzi ni kitu kizuri mbona kuna watu ambao hukosa au hushindwa kupata wapenzi ? Nakubali kwamba kuna watu ambao wenyewe huamua kusalia single ,wana sababu zao na ni busara kuziheshimu . Wanaolengwa hapa ni wale ambao wanataka kuwa katika uhusiano lakini wamefeli,wamekosa kupata wenzao au wameshindwa kudumisha uhusiano.
Hizi ni baadhi ya sababu ambazo huenda zinakufanya unasalia kuwa Single .
1.Kuogopa kuvunjwa moyo
Aghalabu wengi hutumia historia ya masaibu ya kale waliopitia kuamua mkondo wa hatua na maamuzi yao .Kwa sababu uliwahi kuvunjwa moyo mara moja au kushuhudia unayemjua akiteswa moyo na masuala ya mapenzi usije ukajitia katika kisanduku cha upweke kwa sababu ya hilo .Wengi hukutana na kutangamana na watu ambao wanaafikia maazimio yao ya uhusiano ila kwa sababu ya woga wa kitakachofuatia ,wanajipata wamebanwa na hofu na kusalia kimya . Umeskia na kusoma zaidi ya mara moja kwamba ‘Nilipenda mara moja na nikafadhaishwa kwa hivyo ,siwezo kupenda tena’. Upuuzi! Maisha hayawezi kuelekezwa na wimbi la hofu kila wakati . Wanaofaulu katika lolote ni wajasiri na hata wakiangushwa mara moja ,safari yao huanza tena upya.
2.Kutojiamini
‘Self esteem’. Jambo hili huanza unapobalaghe wakati maungo yako na maumbile yanapoanza kubadilika .Maajuzi nimekutana na mwanadada mrembo wa kutisha ,ila mtoto wa kike ameniambia kwa upole na huruma kwamba hawezi kuvalia rinda! Sababu? Eti rafiki zake walimwambia kwamba umbo lake sio zuri akivalia rinda.Argh. Hiki kimemfanya maskini Naomi hajiamini machoni pa wanaume akiwa amevalia rinda .Anafikiria hapendezi na kumbe kauli ya rafiki zake ilikuwa potovu .Vitu vichache na dhana zisizo na msingi ni baadhi ya vinavyotufanya tukose kujiamini . Najua hakuna aliye na uhalisi . No One is perfect ! lakini jamani usije ukajizika kwa sababu ya kukosa kujiamini kwa lolote . Kuna watu ,wanawake kwa wanaume wanaofikiri kwamba hawana hadhi ama uwezo wa kupenda au kupendwa na mtu fulani .Jipe fursa angalau !
3.Kutojijua
Hili ni zito .Jamani hakikisha kwamba unajifahamu kibinafsi .uwezo wako ni upi .Mchango wako katika uhusiano wowote ni upi ? mtazamo wako kuhusu kila jambo ni upi? Ni vipi unajibeba ukiwa faraghani na unapokuwa hadharani? Ni nyakati gani za kusema ukweli na ni zipi za kutumia chembe ndogo za urongo ? Ni mipaka ipi unaweza kujizuia kufanya kisichofaa? Hakikisha kwamba unajifahamu kwa undani kabla ya kutaka uhusiano .Watu wengi hawajijui ndiposa wakati wanapoanza uhusiano ,haufaulu kwa ajili mwenzao huwaambia vitu tofauti sana . Najua ushawahi kusikia kauli hii ya kiingereza-‘S/h’es Not the Person I knew’. Hili hutokana na mtu kutojijua au kutoa taswira isio halisi .Unapokutana na mtu ,kuwa mkweli,kuwa halisi ,kuwa muwazi kuanzia mwanzo .Usije ukamkanganya mwenzako kwa kutoa picha mbili tofauti za ubinafsi wako.Be Real !
Kuchagua/Maringo/ubaguzi/
Sitawafichua wote naowajua ambao waliachwa vinyua wazi hadi leo kwa ajili ya tabia yao ya kutoona uzuri katika kila kitu . Namjua mtu ambaye alitimu umri wa kuolewa lakini kila mvulana aliyekuja kutoa posa alipatikana kuwa na kasoro . Zeina hakukosa kasoro katika kila mwanamme aliyemtaka ..Mara oh… huyu Selemani ana kichwa kikubwa…. Huyu Adamu mzuri kweli ana bidii lakini ni mfupi …… eh …huyu Charles mtanashati kweli lakini ni mweusi …mara huyu Peter ananipendeza lakini ni maskini hohe hahe..na orodha ikawa ndefu zaidi ..na hata sijazidisha chumvi kwa hili .True story . Najua kila mtu ana vigezo anavyoangalia katika mtu anayetamania awe mchumba au mpenzi wake .Lakini basi itakuwa makosa endapo kila sababu yoyote hata iwe nyepesi kama nyuzi kuchukuliwa kuwa kitu kikubwa na kukukosesha fursa . Fahamu kwamba kuna vitu ambavyo unaweza kuishi vyema navyo. Kila unachoona ,hukioni kilivyo-unaona kasoro tu..unanusa udhaifu 100 metres away!
Kuogopa Ushindani
Kuna wasiokuwa na wapenzi kwa sababu ya kuhofia ushidani .Je nikimpenda mtu na kumbe kuna mwengine anayempenda ,nitaweza kumnyakua? Karne hii ,kuna ongezeko na uwezekano mkubwa wa kujipata katika ninachokiita ‘Relationship food chain’ –unakuwa sehemu ya sakata kubwa ya uhusiano na mtu ambaye ana uhusiano kama huo na watu wengine kadhaa.Mwishowe unasalia kuwa tu sehemu ya muundo mkubwa wa mduara unaozunguka kuanzia Januari hadi Disemba bila matokeo ya kuonekana . Kuna wanaoogopa kujipata katika visa kama hivyo vya mapenzi .wanaogopa ushindani uliopo. Kuna mwanamke ambaye hawezi kukubali kwamba mumewe au mchumbake anawavutia pia watu wengine nje .Kuna mwanamme ambaye hawezi kamwe kukubali kwamba mchumbake anawavutia wanaume wengine .Wakati mwingine kufahamu hatari kama hizo katika mahusiano pia huwafanya watu kuamua kuwa single . Lakini iwapo utakuwa mkweli kuanzia mwanzo katika uhusiano wako na ujifahamu,basi huwezi kukosa mtu wa kumpenda kwa sababu ya kuogopa ushindani .Usisalimu amri haraka .
6.Kujitenga/kujiweka pembeni
Umekuwa na mtindo fulani ambao sasa unaweza kutabirika .Mtindo wako wa kuanzia jumatatu hadi jumapili unajulikana na hufanyi kipya ili kujiuza kama anayehitaji au kutaka uhusiano . umejitenga na hutangamani na hata wadudu! Kila chako ni wewe pekee yako! You are riding solo .Itakuwa vigumu sana kupata mtu au kuingia katika uhusiano endapo hii ndio sababu inayokuzuia kuwa katika uhusiano . Kuwa na marafiki ,hudhuria hafla hata zisizohusiana na kazi yako . ‘funua fikra’ na uwe tayari kujithubutu kuwajua watu wapya na wenye mitazamo tofauti na wako. Shiriki michezo au shughuli ambazo ni ngeni kwako ,kubali vipya na kuwa tayari kucheshwa na yalio tofauti .
7.Kujibana kutumia vijikanuni vyetu
Kutafuta mapenzi sio kibarua rahisi ,lakini ni vizuri kujianzia safari hii mwenyewe ili unachoona na kuhisi kiwe ni kutoka kwako . sio cha kuambiwa . ni vizuri kuziepuka tabia au dhana ambazo zimekuwa zinakuzuia kujiacha nje . Mitindo na vijikanuni ambavyo umevitunga kuendesha maisha yako vinaweza kuwa vikwazo vikubwa kwako kupata mtu anayekupenda . Usiogope kuumizwa .Sote tuna udhaifu ,ambao mara nying hudhihirika bayana tunapoanza kumsongea mtu na kumpenda . Kwa hivyo kuafikia kilele cha mapenzi ni safari ya wajasiri na inaridisha sana kwa ajii ya nguvu na kujituma ambako tunadhihirisha ili kupendwa na mtu au kumpenda mtu . Huwezi kujua unajipenda vipi endapo hujawaji kujipa fursa ya kumpenda mtu .Uhusiano wako na mtu mwingine tofauti hujenga Uthabiti wa kindani wa uhusiano wako na wewe mwenyewe.Love somebody..Please
8.Kutaka vya rahisi /vyepesi
Kwa wakati mwingine ,mambo tuliopitia hutufanya kuwa wavivu kupigania chochote .Hali hii hutufanya tujiambie kwamba kuna njia rahisi ya kumfanya mtu kukupenda .lakini ukweli ni kuwa chochote cha kupata kwa urahisi hakidumu . Uhusiano wowote wa kudumu huchukua muda na ni kazi nzito. Huhitaji kujitolea na uvumilivu .Vyote hivi ni vigumu na hivyo basi wengi hujipata na jaribio la kutumia mkato kupendwa . Usiseme wongo; wongo baadaye utakurudi . Usiwe na matarajio kupindukia au yasioweza kuafikiwa-hili litakufanya umchukie mwenzako na kukufanya kutoweza kuwa katika uhusiano .Usikimbilie uhusiano na mtu bila kumfahamu . Wengi hukimbilia ‘vivutio’. Kila mtu ana sifa au mambo yanayomfanya kuwavutia watu kwa nje lakini huenda siye mtu halisi wa kuwa katika uhusiano naye . Njia hizi za mkato na rahisi zinakufanya unajiingiza katika mahusiano yasiokufaa kisha baadaye unafoka kwa ukali maneno kama ‘All men are the same’.Dada ,kwani ulipewa kazi ya kupima sampuli zote za wanaume au ulitaka mapenzi?
0 Comments