Mambo yetu yale, si jambo pekee linaloashiria kwamba wewe na mwenzi wako mko vizuri lakini ni jambo muhimu sana katika kila mahusiano.
Kama katika mahusiano yenu hamridhishani na kama mwanaume ndIo haushughuliki kabisa kitandani, hiyo itapelekea matatizo hata katika mambo mengine kwenye maisha yenu.
Je, ni mambo gani haswa yanakufanya ukose hamu ya tendo kama mwanaume na kuishia kuwa mwanaume suruali maana haukidhi haja za mwenzi wako inavyopaswa? Jibu ni kwamba, tabia zako tu zinaweza pelekea hivo. Zisome tabia hizo hapa chini:
Kula kupita kiasi
Ukijikuta unakula sana na kila mara si tu uzito utaogezea, bali tafiti za Livestrong.com zinaomyesha kwamba aina ya vyakula na kiasi unachokula vinaweza kuleta madhara katika ufanyaji wa tendo la ndoa. Kama kula sana kunapelekea kuongezea uzito kupita kiasi ndo kabisa kutakufanya ushindwe kutoa huduma nzuri kwa mkeo. Hakikisha unakula vyakula sahihi na kwa wakati.
Kunywa pombe kupita Kiasi
Wengi hudhani kwamba pombe ndo inaongeza stimu, lakini hii si mara zote. Tambua kwamba, vinjywaji viwili au hata vitatu vyapombe vinaweza kua sababu ya kutofanya vizuri kitandani, tafiti zinaonyesha, jinsi pombe inavyoongezeka kwenye damu yako, ndivyo jinsi hamu ya kufanya mapenzi hupungua. Hii haimaanishi huache pombe, la, ila jitahidi kupunguza basi. Pombe haikusaidii lolote kwenye sita kwa sita.
Kuchelewa kulala
Je wewe ni mtu wa kuchelewa kulala, kisha unawahi sana kuamka, na kwa maana hiyo kuna masaa muhimu ya kulala unayakosa? Jua kwamba una hatari ya kuua hamu ya kufanya tendo, sababu moja wapo ni masuala ya kihomoni, unapokosa usingizi wa kutosha, mabadiliko katika utengenezaji wa homoni huweza kupunguza matatmanio ya kufanya tendo.
Kingine, kukosa usingizi tu kunaweza kukufanya ujiskie hovyo, na uwe na mudi mbaya, katika hali hiyo kufanya tend au kumhudumia mkeo ni jambo linalokua gumu kulifikiria.
Unywaji wa Kahawa uliopitiliza
Tunapokunywa kahawa huwa hatufikirii madhara yake ambayo hujumuisha madara katika tendo. Kama wewe n impenda kahawa kupita kiasi, si ajabu haufurahii tendo.
Tafiti zinaonyesha, kunywa kahawa kunaweza kuingiliana na homoni zako na kupelekea mwili wako kuzidisha uzalishaji wa homoni nyingi za msongo wa mawazo na kutengeneza homoni chache sana za kuongeza hamu ya tendo. Jitahidi kupunguza matumizi ya kahawa.
Mazoezi kupita kiasi
Mazoezi na utengenezwaji wa homoni vinahusiana na hii inaweza leta matokeo chanya au hasi. Kuna tafiti zinazothibithisha kwamba mazoezi magumu sana kupita kiasi yanakata stimu juu ya ya tendo. Mazoezi tu ya kawaida ni mazuri n ayatakueka katika mudi nzuri ya kufanya mapenzi. Hivyo jua kwamba si kila mazoezi ni mazuri, jitahidi kutafuta uwiano mzuri.
Kutumi muda mwingi na Mwenzi wako
Kuna msemo wa kizungu unasema ‘Sometimes absence make heart grow fonder’ yaani mtu akiwa hayupo unakua unampenda zaidi na kumkumbuka. Jamani, si lazima kila saa uwe na mpenzi wako, hili litakua tatizo kwani hata hamu na mwenzio itapungua mwisho wa siku utaonekana mwanaume suruali.
Wanasaikoojia wanashauri kujitahidi kutenga muda wakutumia na mwenzi wako, lakini pia kuweka muda wa kuwa mbali nae. Kwa kufanya hivyo utajikuta una hamu na mwenzi wako na hautakua na presha ya kufaya kila mara kama mnavokua pamoja mda wote.
0 Comments