NINI HUTOKEA PALE MWANAMKE ANAPOKOMA HEDHI???

Mwenendo wa afya zetu zinachangiwa na aina ya watu tunaoambatana nao ikiwemo marafiki, wapenzi na ndugu pia, kama watu wa karibu yako ni sumu na wanakujaza maneno hasi basi tegemea afya yako kuzorota na kuumwa kila siku pasipo kuwa na dawa ya kumeza ili kutibu tatizo husika. Umewahi kwenda hspitali na kupimwa kisha Daktari kukwambia huna tatizo lolote la kiafya? , jibu ni kwamba unaweza ukazingatia taratibu zote za kiafya kama kufanya mazoezi, usivute sigara wala kunywa pombe, na kuhakikisha uzito wako uko vizuri lakini mahusiano yako yakawa mabaya na kupelekea kupata msongo wa mawazo  basi ni lazima utapata maradhi na kuongeza hatari ya kuugua.

Nini kinatokea pale mahusiano yanapoharibika

Kwa watu wengi mahusiano ni chazo kikubwa cha msongo wa mawazo, ni wazi kwamba mahusiano hubadilika kadiri tunavokua na tunavobadili mienendo ya kimaisha, marafiki zako na familia wanaweza kushangazwa na tabia au mwendendo mpya ulionao.

Nini kinatokea pale mwanamke anapokoma hedhi?

Kukoma hedhi au kwa kitaalamu menopause ni hali ya kawaida inayomtokea kila mwanamke, pale kupata hedhi kunapofikia kikomo na hivo uwezo wa kupata mimba au ujauzito kushuka na kukoma kabisa. Hatua hii hutokea pale mwanamke anapofikisha umri wa miaka 50 na kuendelea, kwa wanawake wengine hali hii hutokea pia kabla ya hapo kuanzia mika 40. Na inaweza kutokea kutokana na ushauri wa madactari ama kufanyiwa upasuaji mdogo, mfano mifuko ya mayai(ovaries) na mfuko wa mimba (uterus) inapoondolewa  kutokana na athari ya magonjwa mbalimbali kama saratani.

Pale mwanamke anapofikia umri wa kukoma hedhi basi huanza kuona dalili zifuatazo

Joto kupanda mara kwa mara na kupata jasho jingiUkavu kwenye ukeKubadilika badilika kwa mpangilio wa hedhiKuongezeka uzito naMsongo wa mawazo na kubadilika kwa mood yako.

Kuna njia nyingi za namna ya kudeal na ishu hii ya kukoma hedhi, kuna njia za mda mrefu na njia za mda mfupi. Njia nzuri na kuepusha madhara yanayotokana na  kukoma hedhi ni kuekebisha lishe yako na kufanya mazoezi ya viungo. Kwa kuzingatia lishe waliyokula mababu zetu hapo zamani basi utapunguza madhara ya kukoma hedhi kama kuongezeka uzito na kutokwa na jasho jingi hasa kipindi cha usiku.

Tambua kwamba Menopasue/kukoma hedhi siyo ugonjwa

Kama tulivoona hapo juu pale mwili wa mwanamke unapokoma kutengeneza homoni za estrogen na progesterone ndipo hedhi yako itakoma. Wanasayansi huenda mbali Zaidi na kuwaanzishia wahanga wa tatizo hili program ya kurudisha homoni hizi kwa kuwawekea homoni zilizotengenezwa maabara, hufahamika Zaidi kama hormone replacement therapy, njia hii inatazama ishu ya kukoma hedhi kama ugonjwa wakati ni suala la kawaida kabisa linalomkuta kila mwanamke.ukweli ni kwamba kitu chochote kilichotengenezwa kwa mkono wa binadamu hakitafanya kazi sawa na kitu kilitengenezwa halisi kwa ajili ya kazi Fulani kwenye mwili, ndio maan madhara ya kuwekewa homoni hizi ni makubwa Zaidi.

Zifuatazo njia za asili unazoweza kutumia ukiwa nyumbani kwako ili upunguze adha zinazotokana na kukoma hedhi.

Kwanza kabisa kama huna uhakika kama umeingia katika kipindi cha kukoma hedhi nenda hospitali mwabie Daktari wako akufanyie kipimo cha FSH, kifupi cha follicle stimulating hormone, kipimo hichi kinagundua iwapo tez ya pituitary inaonesha iwapo ovari zako hazifanyi kazi inavotakiwa na hivo kuna uzalishaji mkubwa wa FSH. Kama uliwahi kufanyiwa upasuaji wa kufunga kizazi basi huna haja ya kufanya hiki kipimo sababu tayari wewe umeshakoma hedhi na uzalishaji wa FSH utakuwa juu Zaidi. Pale FSH inapokuwa nyingi basi kuna uhakika mkubwa kwamba tayari umeanza kukoma hedhi .kisha baada ya hapo utaingia kipindi cha Post-menopause, ni pale ambapo utakoma kupata hedhi mfululizo kwa mwaka mzima.kumbuka mwanzo tumesema menopause siyo ugonjwa na kitu cha kawiada, lakini matokeo yake unaweza kuyabadili kwa kurekebisha lishe na mtindo wako wa Maisha na ukafurahia Maisha yako.

Tumia virutubisho/supliments kama

Virutubisho vya mafuta ya samaki(fish oil) yenye Omega 3 , vyenye ubora wa hali ya juu, kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika.
Zinc supliments

Kwa wanawake, Madini ya Zinc yanahusika katika ukuuaji wa yai (oocyte). Kama mwanamke atakuwa na upungufu wa zinc, yai halitakomaa vizuri na utolewaji wa yai (ovulation) utazuiliwa , na kusababisha ugumba. Kiwango cha zinc cha kutosha kunamwezesha mwanamke kutumia estrogen na progesterone vizuri.

vidonge hivi vilivyotengenezwa kiasili kwa kutumia viambata vya mimea ya Glycine, Radiz Paeoniae Alba Eztractum na Ganoderma husaidia: kuongeza ufanyaji kazi wa mfuko wa mayai (ovaries), kuzuia Saratani ya matiti na kuimarisha afya ya mifupa kwa wanawake waliokoma hedhi.(menopause).

Hakikisha mlo wako unakuwa na kiasi sawa cha vyakula vya mafuta kwa wingi ikifuatiwa na potini na kisha matumizi ya wanga na sukari kwa kiasi kidogo sanaEpuka matumizi ya vyakula na vinywaji vilivyosindikwa maana huongeza kiasi cha homoni ya estrogen.Hakikisha unakuwa na ratiba nzuri ya kufanya mazoeziili kurekebisha kiwango cha insulin na hivo kusaidia kubalansi kiwango cha estrogen.Pata vitamin D ya kutosha,

miili yetu ina uwezo wakutengeneza vitamin D kutoka kwenye mwanga wa jua, hivo hakikisha kila siku unapata mwanga wa jua walau nusu saa mpaka saa 1 ili kuuwezesha mwili kutengeneza Vitamin D ya kutosha. Tafiti zinaonesha kuwa Vitamin D husaidia kupunguza athari za zinazotokana na kukoma hedhi kama kutokwa na jasho jingi usiku bial kumeza vidonge.Kupunguza uzito husaidia kurekebisha na kupunguza athari za menopause kama kubadilika kwa joto la mwili: tafiti zinasema kwamba wanawake wanaopunguza uzito ama walio kwenye program za kupunguza uzito wana uafadhali katibu 33% Zaidi ya kupunguza athari za menopause kuliko wanawake wengine. Kutokana na kwamba swala la kupunguza uzito huchukua muda mrefu nashauri ujijengee tabia ya kurekisha uzito wako kabla hujafikia kipindi cha menopause.

ni matumaini yetu kwamba utaanza kurekebisha sasa mtindo wako wa maisha ikiwemo lishe , ili uweze kupunguza athari za kukoma hedhi. Kwa ushauri huduma ya virutubisho na maswali usiache kutupigia kwa namba zetu 0762336530 . Email info@lindaafya.com.

Post a Comment

0 Comments