MWANAMKE AMUUA MUMEWE BAADA YA KUKATAA KULA CHAKULA CHAKE

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 45 anazuiliwa katika kituo cha polisi cha sio port kaunti ndogo ya samia kaunti ya Busia baada ya kudaiwa kumuua mumewe.

Mwanamke huyo kwa jina Lilian Wanyama anadaiwa kumuua mumewe na kisha kujaribu kumpa huduma ya kwanza kwa kumlisha unga wa ugali na kupelekea kifo chake.

Mtoto aliyeshuhudia kisa hicho anasema mwendazeke kwa jina Daniel Ombunda wa Miaka hamsini na nane alikuwa na ugomvi na mkewe aliyekuwa mlevi baada ya kukataa kula chakula alichokuwa amewapikia na kuwapelekea kaunza kupigana lakini mama huyo akamzidi bwanake nguvu.

Peter Ombunda ambaye ni ndugu wa mwendazake anasema wawili hao ambao wameishi kwa miaka mitatubaada ya kutengana kwa miaka saba wamekuwa na ugomvi kwa muda mrefu na hata visa hivyo kuripotiwa katika kituo cha polisi cha sio port.

Photo Credits: courtesy

Post a Comment

0 Comments