MSANII wa filamu na video queen maarufu Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’ ameibuka na kueleza sababu za uchumba wake kuvunjika. Kidoa alifikia hatua ya kufungukia hilo kutokana na habari kuzagaa kwamba uchumba wake umevunjika ambapo alisema ni kweli na sababu ni kutokana na tofauti ya dini kwani yeye ni Muislam namchumba wake ni ambaye alikuwa ameshatoa posa na kuishi naye maeneo ya Tabata, Dar ni Mkristo.
“Sababu kubwa ya kuachana na mchumba wangu ambaye alikuwa ameshapeleka posa nyumbanikwetu ni dini, wazazi wangu walinikataza kwa kuwa sisi kwetu ni sala tano, ikabidi niwasikilize wazazi wangu na uchumba kuvunjika hivyo kwa sasa niko singo,” alisema Kidoa.
0 Comments