JINSI YA KUMSIFIA MSICHANA MREMBO KWA KUTUMIA VIONJO VIPYA

Kila siku huwa tunapenda kuwaambia wanawake ni warembo. Neno hili limewaingia katika akili zao kiasi cha kuwa ile maana msingi ya neno ‘wewe ni mrembo’ imepotea. Hii ni kwa sababu baadhi ya wanaume wasiojua kutongoza wanaishia kulitumia neno hili vibaya kiasi cha kuwa neno hili limepoteza uhalisia.

Je ulikuwa wajua kuwa wanawake hupenda kusifiwa? Na ulikuwa ukijua kuwa kumsifia mwanamke mara kwa mara ni njia moja wapo ya kutongoza?  leo tumekuja na mambo tofauti ambayo unapaswa kutumia ili umshawishi mwanamke kuwa ni mrembo, na wala hataona kama ni maneno unalompakizia ama maneno ambayo ameyazoea kuyaskiliza awali.

Twende pamoja:
Jambo la kwanza 
Wakati unapotaka kumsifia mwanamke kuwa ni mrembo, usimwambia, “Wewe ni mrembo” mara kwa mara kwa sababu itafikia mahali flani neno hilo litaisha ladha. Badala yake tafuta sehemu muhimu kutoka kwa mwili wake ambayo utaitumia kama kigezo cha kumsifia. Kwa mfano kama umependezwa na pua yake mwambia, “Nimependezwa na pua yako, kila mara nikiiona najiskia na furaha.” Ama kama umependezwa na mashavu yake unaweza kumwambia, “Mashavu yako ndio nuru ya macho yangu, yanapendeza.” Kumwambia mwanamke maneno kama haya yatamfanya atamani kuwa kando yako. Pia ataona kuwa unamwona anapendeza, unamakinika kuuona urembo wake kupitia kwa viungo vyake vya mwili.

Jambo la pili 
Kumsifia mwanamke urembo wake hakuhusishi ngozi yake ya nje pekee, bali pia sehemu yake ya ndani, yaani nafsi yake. Wanaume wengi huwa wanamakinika kumsifia mwanamke umbo, sura na shepu yake huku wakisahau kuwa nafsi ya mwanamke ina umuhimu. Kumsifia mwanamke kwa ujasiri wake, ubunifu wake, hekma, na ujanja kutakupa mkono wa mbele zaidi wakati unapomtongoza ama unapomshawishi. Jambo hili tulishawahi kulizungumzia katika moja ya hatua ya kumtongoza mwanamke ambaye hayuko ligi sawa na wewe. Kumshawishi na kumsifia mwanamke nafsi yake kutamfanya ajiunganishe na wewe zaidi kuliko mwanamke yeyote yule, hivyo hatua iko kwako sasa.

Jambo la tatu. 
Unapomsifia mwanamke usitumie maneno hayo kwa hayo. Yaani wewe kila siku ukikutana na yeye unamwambia, “Nakupenda, leo umeangaza nafsi yangu.” Matumizi ya neno moja siku nenda siku rudi kutamfanya mwanamke atilie shaka iwapo unasema maneno hayo ndani ya moyo wako ama unasema kumridhisha tu. Well, mbona usije na misamiati mipya? Ama mbona usije na maneno ambayo angetamani kuyaskia? Ukitumia maneno kama ‘hurulaini’, ‘malkia, leo nimekuja kwa milki yako’, ‘ua langu la waridi’ nk kutamfanya mwanamke akupende zaidi na zaidi. So anza kutafuta maneno ambayo anayapenda. Usiingiwe na uvivu wa kutumia maneno hayo kwa hayo kila siku. Kumbuka hapa unataka kuwa bora zaidi kati ya wanaume wale wengine. Chukua hatua sasa.

Jambo la nne 
Wakati ambapo umeamua kumsifia mwanamke kama huyu, hakikisha kuwa unamwangalia machoni. Kama ni mwanamke ambaye ndio unaanza kumfukuzia basi jenga confidence ya kumwangalia machoni. Usimsifie huku ukiangalia pembeni ama kuangalia kando. Kumbuka wewe ni Mwanaume Alpha, na wanaume alpha huwa hawatatiziki kama wanatoa hisia zao kuhusu wanawake wanaowapenda.

Post a Comment

0 Comments