Takwimu, zilizopo sasa zinaonyesha ongezeko kubwa la talaka kwa ndoa nyingi katika nchi za Afrika Mashariki. Ndoa ni jambo la kiimani na ibada kwa jamii zilizo nyingi, lakini kwa sasa zinaonekana kukumbwa na dhoruba, ya ama kutengana ama kutalakiana kabisa. Nchini Tanzania, Utafiti wa kufuatilia kaya Tanzania, wa mwaka 2014/15 uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) unaonyesha kuwa kiwango cha talaka kimeongezeka kwa asilimia 1.1
Hii ina maana kuwa kwa sasa kila watu 100 wenye umri wa kuoa au kuolewa waliopo Tanzania, wawili wametalakiwa kutoka mmoja mwaka 2008/09.
Mbali na talaka, kuna wanandoa takriban wanne kwa kila 100 ambao wametengana.
Hali hiyo pia inazikumba nchi za zingine za Afrika mashariki Kenya, Rwanda na Uganda.
Kulingana na msemaji wa mahakama za Rwanda Mtabazi Harrison takwimu juu ya kuvunjika kwa ndoa zinaonyesha kuwa tatizo hilo linaendelea kuongezeka.
”Tulipata takwimu zinazoonyesha kuwa idadi ya ndoa za watu wanaotaka kutenganishwa zilikuwa 2236 kuanzia mwezi...
0 Comments