DEMU KAMA HUYU UNAMCHUKULIAJE??

Hivi kwa mtazamo wako tu, unamchukuliaje demu ambaye ana tabia kami hizi na anadai anakupenda kwa dhati na ukimwambia ajirekebishe anaomba msamaha na kuahidi harudii tena ila baada ya muda anarudia. Na pia ukiamua kumuacha analia sana na kuonyesha kudhoofika sana, kila wakati anatuma marafiki kumwombea msamaha, meseji za msamaha na kupiga simu kuomba msamaha kila wakati ila ukimsamehe anarudia tena.....yaani demu mwenye tabia hizi;

1. Ambaye ukipanga kuonana nae kila wakati anadai yupo busy.
2. Ambaye hataki kabisa uguse simu yake 
3. Ambaye ukitaka kwenda kumtambulisha home kwa wazazi anatoa sababu kila siku za kutokuja, yaani anadai yupo busy.
4. Ambaye mambo yake hakuweki wazi, anafichaficha tu.
5. Ambaye ana ahadi hewa.
6. Ambaye maamuzi yake mengi huomba ushauri kwa dada zake au marafiki...yaani mara nyingi yeye sio muamuzi wa Mambo yake.

KWAKO BINAFSI UNAMCHUKULIAJE DEMU KAMA HUYU?
_Mm kwangu naona ni ana mwanaume zaidi ya mmoja,je ww?

Post a Comment

0 Comments