ASUTWA KWA KUMFANYA MUMEWE KIJAKAZI WA NDANI

Kipusa mtaani Huruma, Nairobi alijipata pabaya baada ya kusutwa na rafiki zake kwa kumuachia mumewe majukumu ya jikoni kila walipotembelewa na wageni.

Duru zinaarifu kwamba, mwanadada huyo alikuwa na mazoea ya kuwashughulikia wageni sebuleni wakipiga gumzo huku mumewe akitayarisha mlo jikoni.

Kulingana na ripoti ya Taifa Leo, rafiki zake binti huyo waliamua kumzomea baada ya kushuhudia tabia yake hiyo ikiwa sasa ni mazoea.

"Unawezaje kumwacha mume wako jikoni akipambana na masufuria huku wewe ukipiga pang'ang'a na wageni jamani? Hivi huoni aibu kusengenywa na watu kwa kukwepa majukumu yako kama mwanamke wa nyumba? Ni sharti urekebishe au tutakutenga," marafiki walimwonya.


Hata hivyo, mrembo alijitetea na kusema kwamba hayo yalikuwa makubaliano yao kwani mumewe alikuwa shupavu jikoni.

Hata hivyo, kauli hiyo haikuwaridhisha wenzake ambao walishikilia ni vyema arekebishe.

Post a Comment

0 Comments