la sanaa Taifa (Basata) limelaani kitendo kilichofanywa na msanii Amber Rutty, huku likimkana kuwa siyo mwanachama wao.
Hatua ya Basata imekuja baada ya msanii huyo kusambaza video kwa mara ya pili kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha akijamiiana na mumewe Said Mtopali.
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa wanandoa hao kufanya kitendo hicho, ambapo kuna kesi dhidi yao inaendelea mahakama ya Kisutu wakikabiliwa na kesi ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile, kisha kusambaza video hizo mitandaoni.
Katika taarifa ya Basata iliyothibitishwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Godfrey Mngereza imeeleza kulaani kitendo hicho , huku ikimkana kuwa siyo msanii kwa sababu hajasajiliwa kwao kufanya shughuli za sanaa, kama msanii binafsi au kutoka katika kikundi chochote kinachofanya shughuli hizo.
“Hiyo taarifa ni yetu, kama Baraza tumesikitishwa na kitendo hicho, tuna imani mamlaka zinazosimamia sheria za mitandao zitachukua sheria stahiki kuhusu jambo hilo, ”amesema Mngereza.
Amesema Baraza linawakumbusha na kuwaasa wasanii wote kutumia maendeleo ya teknolojia na mitandao ya kijamii kwa lengo la kujiletea maendeleo badala ya kutumia kusambaza vitu visivyo na manufaa kwa na vinavyowadhalilisha.
0 Comments