Baada ya Video Yake Ngono Kusambaa, Amber Rutty Aanika Waraka
VIDEO queen aliyejipatia umarufu mitandaoni baada ya kuvuja kwa picha zake na video akifanya tendo la ngono na mpenzi wake kinyume cha maumbile, Amber Rutty, amewaijia juu watu wanaomshambulia kwa matusi mitandaoni wakidai kuwa hajaacha tabia yake hiyo.
Ikiwa ni saa chache baada ya kusambaa kwa video nyingine ikiwaonyesha msanii huyo na mpenzi wake wakifanya ngono huku wakijirekodi, Amber Rutty ameandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instagram, baada ya kuendelea kuzagaa kwa video zake za faragha mitandaoni.
“Habari nasikitishwa sana na baadhi ya vitu vinavyofanywa na watu wanaotumia matumizi mabaya ya mitandao kwanjia ya kutaka nionekane mkosefu kila leo ingawa pia najiskia vibaya kuona hata watu wanaotuzunguka nao kushindwa kuchunguza kiundani jambo hili.
“Nakukumbuka suala zima lililowahi kutokea mpaka kupelekea mamlaka husika kutuchukulia hatua na tukajisalimisha kituoni tukasota sana Segerea na mpaka leo bado kesi ipo mahakamani kupitia hizo izo picha /video chafu wanazozisambaza tena kwa mara nyingine tena.
“Sipo hapa kwa ajili ya kutaka kujua anaefanya ivi kusudio lake ni nini kwasababu hata ukitazama mionekano yetu ya sasa nahizo video ukianza na mikono ya mmewangu davil mpaka vidolen ambapo amechora tattoos toka mwaka jana mwezi wa 12 napia atamimi ukijalibu kuniangalia the way nilivyo sasa na hzo video kuna utafauti mkubwa sana.
“Pengine furaha ya mtu anaefanya haya yote ni kuona ndoto zetu zinapotelea gizani au kutaka kuona mmoja kati yetu kapoteza uhai ukizingatia swala tayar lipo mahakaman toka October mwaka jana lakin bado leo hii wanayarudia kuyafufua hayo hayo.
“Kiukweli tumechanganyikiwa kiakili mpaka kiafya atupo sawa ombiletu ni kuomba anaeusika na ili jambo tunaomba aache maramoja kuendelea kwasababu sisi ni binadamu maumivu /mateso tunayoyapitia kwakipindi hiki ni makubwa mno please please.”
Tukio la kuvuja kwa picha hizo mitandaoni zikimuonyesha Amber Rutty na mpenzi wake zilivuja Oktoba 2019. Jana Ijumaa pia zilisambaa video nyingine zikiwaonyesha Amber Rutty na mpenzi wake wakifanya ngono. Hata hivyo BASATA imesema haimtambui kama ni msanii kwani hajasajiliwa kwenye baraza hilo.
0 Comments