ZIJUE FAIDA ZA KUNYWA MAJI KILA SIKU ASUBUHI

Kwanini ni muhimu kunywa maji?

Miili yetu inaundwa na asilimia 70 ya maji, hivyo ni muhimu kunywa maji ya kutosha ili kuufanya mwili kufanya kazi vyema. Iwapo mwili wako haupati maji ya kutosha, hali hii inaweza kusababisha madhara mbalimbali ya muda mfupi na muda mrefu kama vile magonjwa ya shinikizo la damu, saratani pamoja na magonjwa ya figo.

Ninawezaje kutumia maji kama tiba?

Unaweza kutumia maji kama tiba ya matatizo mbalimbali kwa kufanya haya yafuatayo:

Kunywa takriban Mililita 160 za maji kabla ya kuswaki au kula chochote mara tu unapoamka.
Kunywa maji angalau dakika 30 kabla ya kula, lakini si ndani ya dakika 45 baada ya kifungua kinywa, chakula cha mchana au chakula cha jioni.
Kama huwezi kunywa angalau bilauri 4 za maji basi anza na moja kisha ongeza taratibu kadri mwili wako unavyomudu.
Karibu ufahamu faida 8 za msingi za kunywa maji kabla ya kula chochote unapoamka.

1. Huondoa sumu mwilini
Unywaji wa maji mengi husaidia kuondoa sumu mwilini kwani huwezesha viungo kama vile figo kufanya kazi yake vyema. Unapokunywa maji kabla ya kula chochote asubuhi utauwezesha mwili wako pia kujenga misuli na kuzalisha seli mpya za damu.

2. Huboresha metaboli
Metaboli ni mchakato ambao mwilli hutumia vyakula (wanga, protini na mafuta) ili kupata nguvu na kujijenga. Hivyo basi, unywaji wa maji huwezesha mchakato huu kwenda vyema na kuufanya mwili kuwa na afya njema.

Kunywa maji kabla ya kula chochote unapoamka huufanya utumbo kuwa tayari kufyonza virutubisho. Kumbuka, maji ni muhimu kwa ajili ya watoto na watu wazima pia.

3. Husaidia kupunguza uzito
Wapo watu wanaopenda kupunguza uzito wa miili yao kwani uzito mkubwa si jambo zuri kiafya. Yakupasa kukumbuka kuwa unapoamka na kuanza kutumia vinywaji kama vile soda na juisi (sharubati) vitachangia sana kuongeza uzito wako wa mwili.

Utafiti unaonyesha kuwa soda ina sukari gramu 35 na gramu 140 za kalori ikilinganisha na maji ambayo vyote ni sifuri. Hivyo basi, ni vyema ukapendelea kunywa maji zaidi kuliko vinywaji vingine.

4. Huondoa kiungulia na matatizo ya umeng’enyaji wa chakula
Kunywa maji kutakusaidia kuzimua asidi inayopatikana tumboni ambayo ndiyo hupelekea tatizo la kiungulia. Sanjari na hayo unywaji wa maji utarahisisha na kuhimiza mchakato mzima wa umeng’enywaji wa chakula.

Hivyo basi, kama unakabiliwa na matatizo haya ni vyema kuzingatia unywaji wa maji kabla ya kutumia dawa mbalimbali.

5. Huboresha na kuimarisha ngozi
Utafiti unaonyesha kuwa kunywa maji takriban mililita 500 kunarahisisha mzunguko mzuri wa damu katika ngozi. Hivyo basi, hili hupelekea kuondoa sumu mbalimbali katika ngozi na kuiacha ngozi yako katika hali nzuri kiafya.

6. Huhamasisha ukuaji wa nywele bora zenye afya
Upungufu wa maji mwilini una madhara makubwa sana kwa afya yako. Utafiti unaonyesha kuwa ¼ ya uzito wa nywele zako ni maji. Hivyo kutokunywa maji yakutosha kutakufanya kuwa na ukuaji duni wa nywele; pia kutafanya nywele zako kuwa dhaifu.

Kwa ajili ya afya na mwonekano bora wa nywele zako jidahidi kunywa maji yakutosha hasa unapoamka asubuhi.

7. Huzuia mawe kwenye figo
Unywaji wa maji huzimua asidi inayosababisha mawe kwenye figo ambayo hupatikana tumboni. Unywaji wa maji ya kutosha kutakuepusha kwa kiasi kikubwa na matatizo ya figo.  Ili kurahisisha utendaji kazi wa figo zako pamoja na afya yake, zingatia kunywa maji ya kutosha hasa asubuhi.

8. Huongeza kinga ya mwili
Kujijenga kwa kinga mwili hutegemea sana maji katika mwili wako. Hivyo ni vyema kuhakikisha unaongeza kinga ya wili wako kwa kunywa maji ya kutosha hasa kabla ya kula kitu chochote.

Neno la mwisho

Ninakuhimiza kujenga utamaduni wa kujali na kulinda afya yako ili uweze kuwa mtu mwenye mafanikio zaidi. Tumeona swala la unywaji wa maji lilivyo na umuhimu

Post a Comment

0 Comments