Unatafuta njia za kupunguza uzani bila kwenda gym kwa sababu ya shughuli za kikazi ,shule au umebanawa kabisa ?
Usiwe na wasi wasi kwani kuna mazoezi mepesi unayoweza kufanya ili kuafikia malengo yako ya kuthibiti uzani .
Fanya mazoezi ya kurukaruka na kujishashua ‘ Aerobics’
Aerobics ni aina ya mazoezi yanayokuwezesha kuufanyisha moyo harakati za kufanya kazi vyema .unaweza kushiriki uogeleaji ,kutemebea ,kuendesha baiskeli na kadhalika .
Mazoezi hayo kwa jina cardio huweza kukusaidia kumaliza mafuta mwilini
Unaweza kuyapata mazoezi ya aerobics kupitia video za youtube au katika warsha za mazoezi . huhitaji kwenda gym kwa hilo.
Planks
Haya ni mazoezi ya kufanya mwili thabiti .yanasaidia kumaliza mafuta katika sehemu ya tumbo .unaweza kuyafanya mazoezi haya baada ya kazi au hata nyumbani .utahitaji tu kuyashiriki kwa sekunde 30 kwa seti mbili .kwa mwezi mmoja tu utaanza kuona tofauti kubwa .
Jumping jacks
Haya ni mazoezi rahisi ya kuruka ambayo unafaa kuyafanya ukibadilisha kiwango cha nafasi kati ya miguu yako huku mikono yako ikiwa juu . unayaweza kuyafanya mara 50 katika seti mbili na utahisi uwezo wake .
Kudensi
Kudensi ni mazoezi yanayohusisha mwili mzima na pia yanapendeza . ni mazoezi bora sana kwa moyo wako na pia yanakusaidia kuainisha voungo vya mwili .
Unaweza kufanya mazoezi haya ni rafiki zako au familia mnaposikiliza muziki na pia kuchoma mafuta wakati huo huo . ni jambo linalosajili faida mara dufu .
Lunges
Lunges ni mazoezi yanayosaidia kulainisha muonekano wa sehemu za chini za mwili ili kukupa nguvu zaidi . pia yanakusaidia kuondoa mistari ya ufuta inayojiwamba kwenye ngozi yaani cellulite .
Unaweza kufanya seri 10 ya mazoezi haya kila siku kwa mwezi mmoja ili kushuhudia matokeo .
Squats
Haya ni mazoezi ya sehemu za chini za mwili yanayolenga kuimarisha misuli ya miguu , paja na sehemu ya nyuma .
Unaweza kuyafanya mazoezi haya popote wakati wowote .seti 25 kila siku ni kiwango bora .
0 Comments