WANAWAKE: MAMBO UNAYOPASWA KUYAJUA KABLA YA KUOLEWA

Naomba kuleta kwenu mambo ambayo naamini ni muhimu kuyatafakari na kuyapa uzito wenye kustahili.

Yafuatayo ndiyo mambo ambayo unapaswa kuyazingatia kabla na baada ya kuolewa:

1. Kujitambua

Kila msichana aweze kutambua nini kinamfanya kuwa mwanamke. Kwa maana kama ni maumbile hiyo ni default settings, kama ni kuzaa mwanaume haendi leba, sasa ni nini kinakufanya kuwa mwanamke? Kujitambua, kujiheshimu na kuwajibika. Nyumba yenye mwanamke anayeheshimika ni Baraka na nyota njema. Nyumba yenye mwanamke asiyejiheshimu na kuheshimika huwa haitamaniki, wewe wataka kuwa yupi kati yao?

2. Kila mwanaume ni tofauti

'wanaume wote ni wale wale tu'' Ni vibaya sana kumchukulia mwanaume sawa tu na wengine (hata kwa rafiki wa kawaida tu). Kuwa unajua au umesikia sifa mbaya za wanaume flani na flani, au umewahi kuwa na mahusiano na ukaona sifa mbaya kadha wa kadha za huyo, ukaja ukampata mwingine harafu unamchukulia ni sawa na hao wengine tu. (kosa kubwa sana) Kila mwanaume ana sifa zake na mapungufu yake. Sifa na mapungufu ya mmoja sio sawa na mwingine.

3. kuamua kuolewa au kutokuolewa

Uamue kama unajiona una wito wa kuolewa au la, tena uamue kwa utashi wako mwenyewe. Usipokuwa umeamua unakosa nafasi adhimu ya kuwa umejianda kuwa chini ya mume na utaona kama unaonewa vile!! Mabaya aliopitia mama au jirani yako kwa mumewe isiwe ndio determinant factor kwa huwa hutaolewa kwani utaolewa na huyo mtesaji au huyu unayemchukia?

Hakika Utaolewa na mwanaume mwingine mwenye sifa na tabia tofauti na kila kitu tofauti na hao, kwa nini uwatumie hao kama ndio wawakilishi wa wanaume wote na ndio wako hivyo? Kwa nini wengi wenu msijifunze kwa wanawake waliofanikiwa kwenye ndoa kuliko hao role models wa kwenye taarabu na saluni? tunajifunza kutoanguka kwa walioanguka iweje hao walioshindwa ndoa ndio wawe chachu kwako? si unajua ni wanawake wachache sana wanapenda kuona mwenzake akifanikiwa?? wengi wanapenda mabaya au shimbo alioanguka na mwenzake nae aanguke hapo.

5. Dhana ya haki sawa

Binafsi naamini kila binadamu ni sawa, ila linapokuja swala la mume na mke huwa nashindwa kuelewa ni haki zipi izo zinazopiganiwa wakati katiba ya nchi haitamki jinsia kwenye haki na stahili?. Au mnataka mke akiwa anakata kitunguu mume awe anakata nyanya?? Mwanamke anapewa heshima ya kuwa msaidizi wa mume. Kuna umuhimu sana wa kutambua na kuchukua nafasi yako kama mwanamke. Beijing waache na wabeijing wenzao. Mwanaume ni Kiongozi wa Mkewe na familia nzima (sifa ya kiongozi- anajali- anawatanguliza wenzake, anasikiliza, anashaurika, anaona mbele, anawajibika, hekima na busara etc)

6. Kujua kupangilia matumizi

Kwa pesa ya familia ya yake kwa ajili ya matumizi binafsi "spending wisdom'' sio kila nguo mpya unayo, msuko mpya unao, kiatu kipya unacho, saa mpya unayo, mkufu mpya unao, kulikoni kwani, Kwa kile kingi au kidogo mnachojaliwa, kitumieni kwa hekima na shukrani.

Post a Comment

0 Comments