WANAOCHAGUA WANAUME WA KUWAOA SOMENI HAPA

 NA HAJI NASSOR, PEMBA

NI haki ya kidini na hata kikatiba kila mmoja, kujenga uhusiano na mtu wa jinsia nyingine, na kwa baadhi ya dini kisha kufuatiwa na neno ndoa.

Suala la kuchangua na kutafuta mwenza kwenye uhusiano wa ndoa, ndio hasa lilanotakiwa, na sio kulitafuta jitu lisilokuwa na maadili au dini maana yapo mengi ya ajabu yanaweza kukutokezea ndani ya mahusiano au ndoa.

Walishasema wazee wetu kwamba, viwili vyachagulika, sembuse vikiwa vingi, ingawa nao muda wa kuchagua unapokwenda mno ni jambo la kuzingatia pia.

Wapo wanawake, pengine kwa kutokua na sababu za msingi sana, wamekuwa wataalamu wa kuchagua waume kila anapoendewa na mwanamme kwa lengo la kufunga nae ndoa.

Ni sawa hili kwa wanawake kuwa makini, lakini usia wangu mnapochagua waume wa kufunga nao ndoa, msisahau kuangalia na umri wenu, maana binadamu sio samaki.

Inaaminika kuwa, samaki kadiri Muumba anavyompa umri mkubwa, ndio na nguvu hata za kizazi nazo huongezeka, ingawa kumbe ni tofauti na mwanadamu na jamii nyingine ya wanyama.

Wataalamu wetu wa afya ya mwanamke, wanasema umri sahihi wa kuanza kuzaa kwa mwanamke ni kuanzia miaka 18 hadi 40 na wengine wakisema hata 49, ingawa wengine wakaenda mbali zaidi kuwa, hata umri huo ni vigumu kupata athahari za kiafya.

Kumbe, lazima wanawake wanaochagua waume na pengine pasi na sababu zinazoingia akili, lazima waangalie na vyeti vyao vya kuzaliwa, kama hawajaavuuka miaka 49.

Haina maana kuanzia miaka 49 ndio kizazi kimeshaondoka moja kwa moja, lazima kudra ya Muunga ipewe nafasi, lakini umri mzuri, sahihi, mwafaka na unaoshauriwa na wataalamu wetu na hasa wa afya ya uzazi kwa wanawake ni kati ya miaka18 hadi 40.

Wapo wanawake wanahitaji kuolewa na wanatamani siku moja awe na watoto wake angalua tisa au 12, lakini anaorodha ya wanaume wasipungua watano hadi 10, ameshawarejesha, kwamba hawamfai.

Duuu….sawa inawezekana umebahatika wote waliokuja kukuchumbia walikuwa ni wizi, walevi, wala unga, majambazi au matapeli tena wa mitandao, sababu hizi zinaingia akili, lakini kama ni kwasababu tu hana gari, angalia umri wako dada.

Ndio, maana wapo wengine ijapokuwa umri wao umeshafikia alaasiri, lakini wapoendewa na wachumba kwa lengo ya kufunga ndoa, masuali huwa hivi….wewe unanyumba ngapi, unakazi gani, huishi kwenye visiwa vidogo, una gari na mengine yasioingia akili.

Sasa wewe unaetafuta muume kondakta wa ndege au, anaefanyakazi ubolozi wa Dubai ama Marekani, je umeshaangalia umeri wako, bado umo kwenye watu wanaotarajiwa kuzaa.

Tena kumbe sayansi inakubali kabisa kuwa, mwanamke akishafika umri wa miaka 26 shingo ya kizazi au kwa lugha nyepesi ‘mlango wa kizazi’ huanza kujibana bana taratiiibu, na hapo sasa akipata ujauzito, kuzaa bila ya tabu huwa ni vigumu mno.

Maana kunzia chini ya umri wa miaka 26, malngo wake wa kizazi, huwa madubuti na imara na uko tayari kwa ajili ya kubeba mimba na mtoto kuzaliwa akiwa salama, kama alivyo mama yake, lakini duu…kunzia miaka 26 hapo mtihani.

Wapo wanawake wanaojifananisha na pacha mwenzake wa kiume, kwamba mbona yeye hajao hadi leo, laa..hashaa mwanamme anaweza kukomea hadi miaka 80 au kupindukia na bado akipata mchumba, mahari yakajibu ndani muda mfupi.

Maana tofauti na mwanamke kwamba, kuanzia miaka 45 tena huko kisayansi kizazi huanza kupotea taratibu, maana wao wanafuko la kubebea kiumbe, na umri ukiwa mkubwa nalo huzeeka.

Yote kwa yote, kuchagua muume sawa….. lakini kama mna nia ya kutafuta na watoto kwenye ndoa, angalieni na umri wenu maana wewe sio samaki ni binadamu.

Viongozi wetu wa dini na madaktari, haya jaribuni kuyaeleza na kuyatolea ufafanuzi kila wakati, maana wapo wanawake wanaodhani kwamba, kuwa digree, PHD, mshahara mnene, nyumba ya kisasa na gari la maringi manene ndio ‘dill’

Hata wanafamilia, kaka, ami, mjomba na mababu sio vibaya hata kidogo, kuwaelimisha watoto na ndugu zetu wa kike, kwamba, msingi na heshima yao ni kuwa katika ndoa, au kwa wale wa dini nyingine ni kuwa na kuwa watoto.

Ingawa imeshaelezwa na watunga mashairi kuwa, kuolewa ni sheria na kuzaa ni maajaliwa, hili halipingiki, lakini kila alimae kwa wakati anategemea kuvuna.

Post a Comment

0 Comments