VYAKULA VINAVYOONGEZA AKILI KWENYE UBONGO

Tunatakiwa kuzingatia suala la ulaji wa vyakula na kujali afya zao kwa kula vyakula vya kujenga mwili na akili pia.  Utamaduni huu ni msaada mkubwa kwa vizazi vijavyo vitakavyozaliwa.

Wataalam mbalimbali na wanasayansi wamekubali kuwa ulaji wa vyakula vifuatavyo ni muhimu sana kwa binadamu na katika kuzingatia hilo ASILI ZETU imekuletea orodha ya vyakula vinavyoongoza kuimarisha utendaji kazi mzuri wa ubongo.

(1). MAFUTA YA SAMAKI : Ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa fahamu, ulaji wa samaki hasa wenye minofu kama vile samoni na dagaa itakusaidia kuongeza akili kwenye ubongo wako kutokana na kuwa na kiasi kingi cha mafuta ya OMEGA 3 ambayo huimarisha utendaji kazi wa ubongo na seli za mwili moja kwa moja.

(2). PILIPILI KALI : Hiki ni chakula kikubwa cha ubongo kwani zinakiwango kikubwa cha vitamini C ambayo huitajika zaidi kwenye ubongo.  Pilipili inaaminka kuwa na kiwango kikubwa cha Vitamini hivyo kuliko hata machungwa.

(3). MBEGU ZA MABOGA : Hizi zina kiwango kikubwa cha madini ya Zinc ambayo husaidia kuongeza kumbukumbu.  Zipo njia nyingi za kula mbegu za maboga mojawapo ni kuzikaanga na kula kama karanga, ukila kiasi cha kiganja kimoja tu kwa siku inakuwa ni vizuri.

(4). NYANYA : Huzuia magonjwa ya ubongo kutokana na kuwa na kirutubisho cha kuweza kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea.  Hivyo ulaji wa nyanya hasa za kuiva utakusaidia kukupa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali yakiwemo ya akili.

(5). KARANGA : Aina zote za karanga mbichi na kavu zina Vitamini E ambayo huzuia tatizo la upotevu wa kumbukumbu na pia zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.

Hivi ni baadhi ya vyakula ambavyo ukivitumia kwa ufasaha utashangaa kuona afya ya ubongo na kumbukumbu zikiimarika kwa kiwango cha juu, wale wenye kuitaji dawa za mitishamba na asili za kuongeza maarifa darasani au biashara, piga : +255 659 32 10 90 au wasiliana nasi kwa barua pepe : asilizetu@gmail.com

Post a Comment

0 Comments